Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yataka hatua za dharura kupunguza madhara kwa mgonjwa wakati wa matibabu

Mgonjwa anaandaliwa kwa ajili ya matibabu ya saratani katika hospitali huko Kandy, Sri Lanka
Petr Pavlicek/IAEA
Mgonjwa anaandaliwa kwa ajili ya matibabu ya saratani katika hospitali huko Kandy, Sri Lanka

WHO yataka hatua za dharura kupunguza madhara kwa mgonjwa wakati wa matibabu

Afya

Mamilioni ya watu wanaathiriwa kila mwaka kutokana na huduma za afya zisizo salama kote duniani, hali inayosababisha vifo vya watu milioni 2.6 kwenye nchi za kipato cha chini na zile za kipato cha wastani.

Asilimia kubwa ya vifo hivi vinaweza kuzuiwa. Athari za kijamii  na kiuchumi zinazotokana na matatizo kwa mgonjwa huchangia kupotea kwa matrilioni ya dola kote duniani.

Shirika la Afya Duniani sasa linaangazia  dunia nzima katika suala la usalama kwa mgongwa na kuzindua kampeni kuhusu uzalendo kwa mgonjwa wakati wa maadhimisho ya kwanza ya siku ya mgonjwa terehe 17 Septemba.

Hakuna mtu anayestahili kuathiriwa wakati akipata huduma za afya. Kote duniani takriban wagonjwa watano hufariki kila dakika kutokana na huduma za afya zisizo salama, alisema Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus, mkurugenzi mkuu wa WHO.

Wagonjwa wanne kati ya kumi huumia wakati wanapata huduma za afya ambapo makosa mengi huhusu vipimo, kutoa dawa na matumizi ya dawa.

WHO inasema makosa kwenye madawa pekee hugharimu takriban dola bilioni 42 kila mwaka. Huduma za upasuaji zisizo salama huleta matatazo kwa hadi asilimia 25 ya wagonjwa na kusababisha vifo vya watu milioni moja wakati au mara tu baada ya upasuaji

Kuumia kwa wagonjwa wakati wa kutoa huduma za afya haikubaliki. WHO inatoa wito wa hatua za dharura kwa nchi kote duniani kupungza madhara kwa wagonjwa wakati wa kupata huhuma za afya.

Uwekezaji katika kuboresha usalama wa mgonjwa unaweza kuokoa fedha. Gharama ya  kuzuia ni ya chini kuliko ile ya kutoa matatizo baada ya kasoro kutokea.

Kama mfano, Marekani pekee iliangazia katika kuboresha hatua iliyochangia kuokoa dola bilioni 28 kwenye hospitali kati ya mwaka 2010 na 2015.

Tarehe 17 Septemba ilibuniwa kama Siku ya Mgonjwa Duniani na mkutano ya 72 wa baraza la afya duninia mnamo Mei 2019.