Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi dhidi ya vituo vya mafuta Saudia vinaiweka Yemen katika nafasi mbaya kwenye ukanda huo-Griffiths

Mark Lowcock mkuu wa OCHA akihutubia Baraza la Usalama kuhusu hali nchini Yemen.
UN Photo/Manuel Elías
Mark Lowcock mkuu wa OCHA akihutubia Baraza la Usalama kuhusu hali nchini Yemen.

Mashambulizi dhidi ya vituo vya mafuta Saudia vinaiweka Yemen katika nafasi mbaya kwenye ukanda huo-Griffiths

Amani na Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limejulishwa kwamba mashambulizi dhidi ya vituo vya mafuta nchini Suadi Arabia mwisho wa wiki yaliyodaiwa kutekelezwa na wapiganaji wa Houthi ni ishara ya kwamba nchi hiyo iliyoghubikwa na machafuko huenda ikakumbwa na machafuko zaidi.

Akihutubia Baraza hilo kwa njia ya video kutoka Amman nchini Jordan, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen, Martin Griffiths amesema, “shambulizi dhidi ya vituo vya ARAMC nchini Saudi Arabia Jumamosi Septemba 14 mwaka huu, ambalo limesambaratisha uzalishaji wa mafuta nchini Saudia una athari hadi nje ya ukanda huo.”

Griffiths amesema, “katika kiwango kidogo, vitendo kama hivyo vinaiweka Yemen katika nafasi mbaya kwa sababu kitu kimoja ambacho tunakifahamu ni kwamba tukio hilo linaongeza uwezekano wa mzozo wa kikanda kuwa mkubwa zaidi na uwezekano wa mahusiano mazuri kuwa mdogo.

Kwa upande wake Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA Mark Lowcock amesema, “tunashuhudia mashambulizi ya mara kwa mara nchini Yemen ambayo yanasababisha mauaji na majeraha kwa raia na uharibifu wa miundombinu. Usitishaji wa mapigano nchini kote kama ninavyopendekeza kwa muda, unaweza kupunguza hatari kwa watu. Pande husika zinahitaji kuzingatia wajibu wao chiini ya sheria za kimataifa wakati wote.”

OCHA inakadiria kwamba takriban asilimia 80 ya idadi ya watu milioni 24 nchini Yemen wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Bwana Lowcock anasema mazingira ambayo watoa huduma za misaada wanafanya kazi nchini Yemen huenda haijawahi kuwa mbaya zaidi ya hali ya sasa.

Idadi kubwa ya matukio ya ufikiaji ilikuwa (Hapa sijaelewa) kutokana na vikwazo vilivyowekwa na wahouthi ambao sheria zao zinakiuka sheria za kibinadamu, amesema Lowcock huku akitaja pia kasi ya serikali kupitisha miradi ya mashirikia yasiyo ya kiserikali.

Bwana Lowcock amekaribisha msaada wa dola milioni 500 kutoka kwa serikali ya Saudia huku akisisitiza umuhimu wa msaada wa kibinadamu kutoka kwa jumuiya ya kimataifa ambao wayemen wanategemea.