Tunahitaji kukomesha mabadiliko ya tabianchi:UN

14 Septemba 2019

Tunahitaji kuhakikisha tunakomesha mabadiliko ya tabianchi amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres baada ya kurejea kutoka Abaco katika visiwa vya Bahama ambako kumeathirika sana na kimbinga doriani.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara hiyo katibu Mkuu amesema alichokishuhudiani hali mbaya, ambayo haikusababishwa na shetani bali mabadiliko ya tabianchi ambayo sasa yanatokea mara kwa mara na yakiwa na nguvu kubwa kupita kiasi.

Amesiitiza kwamba “Mosi ni lazima kukomesha mabadiliko ya tabia nchi. Tunahitaji kuhakikisha kwamba tunabadili mwenendo wa sasa mahali ambako mabadilikoya tabianchi yanakwenda kasi kuliko sisi. Na pili nchi kama Visiwa vya Bahama ambayo sio mchanganiaji wa mabadiliko ya tabianchi lakini iko mstari wa mbele kuathiriwa vibaya na mabadiliko hayo inastahili msaada wa kimataifa ili kuweza kukabiliana na dharura ya kibinadamu iliyowapata , lakini pia ijenzi mpya na kuzijengea mnepo jamii zake na visiwa vyake.”

Ameongeza kuwa hadi sasa kumekuwa na mshikamano mkubwa wa serikali ya visiwa vya Bahama, watu, nchi mbalimbali, jumuiyaya kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya kimataifa.

Yanafanya kila liwezekekanalo kwa ukarimu mkubwa kazi ya kuwasaidia maelfu ya watu walioathirika. Lakini msaada huo unahitaji uwekezaji mkubwa na visiwa vya Bahama vinahitaji kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa ili kukabiliana na athari za zahma ya mabadiliko ya tabianchi na kujijenga upya.

Pia Katibu Mkuu amesema “Tuna mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa ambayo yanashirikiana na serikali na wadau wengine kutoa msaada. Na tumekuwa tunashirikiana na serikali tatu za Varibbea kuwasilisha mapendekezo yenye lengo la kujikita na uwekezaji na kujenga mnepo na ujenzi mpya.

 

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud