Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shmbulio dhidi ya kituo cha mafuta Saudia linatutia hofu:Griffiths

Martin Griffiths
UN Photo/Manuel Elías
Martin Griffiths

Shmbulio dhidi ya kituo cha mafuta Saudia linatutia hofu:Griffiths

Tabianchi na mazingira

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Martin Griffiths amesema anatiwa hofu kubwa kuhusu mashambulio yaliyofanywa na ndege isiyo na rubani au drine katika vituo viwili vya mafuta kwenye Ufalme wa Saudi Arabia.

Kundi la Ansar Allah limekiri kuhusika na shambulio hilo la leo ambao bwana Griffiths anasemma mvutano wa kijeshi wa hivi karibuni unaleta wasiwasi mkubwa.

Kupitia taarifa yake mwakilishi huyo maalum wa Yemen ametoa wito kwa pande zote kujizuia na mvutano zaidi na kuzitaka pande zote kuepuka matukio Zaidi kama hayo ambayo yanatoa tishio kubwa kwa usalama wa kanda nzima , kufanya hali ambayo tayari ni mbaya kuwa mbaya Zaidi na kuuweka njia panda mchkato wa kisiasa unaosimamiwa na Umoja wa Mataifa.