Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatuma wataalamu wake nchini Tanzania kusaidia uchunguzi wa uvumi kuhusu ugonjwa ambao haujajulikana

Katika picha ya maktaba ni mtaalamu wa WHO akifanya uchunguzi
WHO/S.Ramo
Katika picha ya maktaba ni mtaalamu wa WHO akifanya uchunguzi

WHO yatuma wataalamu wake nchini Tanzania kusaidia uchunguzi wa uvumi kuhusu ugonjwa ambao haujajulikana

Afya

Shirika la afya duniani WHO kupitia ukurasa wake wa tovuti kanda ya Afrika mjini Brazzaville, Congo, limesema kwa kushirikiana na mamlaka ya afya nchini Tanzania wanapeleka timu ya wataalamu nchini humo kuchunguza fununu za kifo cha mtu mmoja kutokana na ugonjwa ambao haujajulikana bado.

WHO imewasiliana na wizara ya afya nchini Tanzania kupata taarifa zaidi na ikaelezea utayari wa kusaidia.

“Sambamba na wajibu wetu chini ya kanuni za kimataifa za afya, WHO mara kwa mara inapokea na kuchunguza uvumi wa masuala ya afya ya umma. Kwa msingi huo, WHO kwa kushirikiana na mamlaka inatuma wataalamu nchini Tanzania kuchunguzi uvumi huo kama jambo la haraka.” Imesema sehemu ya taarifa hiyo.

WHO itawasilisha matokeo ya uchunguzi kwa nchi wanachama.