Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya yazindua chanjo ya malaria, ugonjwa unaoua mtoto mmoja kila baada ya dakika mbili

Afisa wa utibabu  akiwa anajitayarisha kupa damu kuona kama ina malaria.
PAHO/WHO Photo
Afisa wa utibabu akiwa anajitayarisha kupa damu kuona kama ina malaria.

Kenya yazindua chanjo ya malaria, ugonjwa unaoua mtoto mmoja kila baada ya dakika mbili

Afya

Shirika la afya duniani WHO limeipongeza serikali ya Kenya kwa kuzindua leo chanjo ya kwanza duniani dhidi ya malaria katika Kaunti ya Homa Bay, magharibi mwa Kenya. 

Programu ya majaribio ya chanjo ya malaria hivi sasa inatekelezwa kikamilifu barani Afrika ambapo Kenya inaungana na Ghana na Malawi kuanzisha chanjo hiyo silaha dhidi ya ugonjwa ambao unaendelea kuwaathiri mamilioni ya watu husuisan watoto barani Afrika.

Chanjo hiyo inayofahamika kama RTS,S, itakuwa kwa ajili ya watoto wa kuanzia umri wa miezi sita katika maeneo yaliyochaguliwa nchini humo kwa ajili ya majaribio ya hatua kwa hatua. Ni chanjo ya kwanza nay a pekee  mahususi kwa ajili ya kupunguza malaria kwa watoto, pamoja na kudhibiti ugonjwa huo unaotishia maisha kwa ujumla.

WHO inasema malaria inaua mtoto mmoja kila baada ya dakika mbili. Ugonjwa huo ndiyo unaoongoza kwa kuua watoto chini ya miaka mitano nchini Kenya.

Matshidiso Moeti ambaye ni Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika amenukuliwa akisema, “Afrika imeshuhudia ongezeko la hivi karibuni la visa vya malaria na vifo. Hii inatishia mafanikio ya mapambano dhidi ya malaria yaliyofanyika katika miongo miwili iliyopita. Jaribio linaloendelea litatoa taarifa muhimu na data kuitaarifu sera ya WHO matumizi mapana ya chanjo katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara. Ikitumika katika eneo pana, chanjo hii ina uwezo wa kuokoa maelfu ya maisha.”

Akizungumza katika tukio la leo lililohudhuriwa na maafisa wa afya, viongozi wa kijamii na wanaharakati wa masuala ya afya, mwakilishi wa  WHO nchini Kenya Dkt Rudi Eggers amesema, “ chanjo ni silaha muhimu ambazo kwa ufasaha zinawafikia na kulinda vizuri afya za watoto ambao wasingeweza kuwafikia kwa haraka madaktari, manesi na vituo vya afya ambao wanatakiwa kuokoa maisha wakati ugonjwa unapokuja. Hii ni siku ya kusherehekea tunavyoanza kujifunza zaidi kuhusu kile ambacho chanjo hii inaweza kufanya kubadili njia ya malaria kupitia chanjo kwa watoto.”

Lengo la chanjo hii ni kuwafikia watoto 120,000 kwa mwaka nchini Kenya katika maeneo yalichogaliwa kwa sasa ikiwemo kaunti ya Homa Bay, Kisumu, Migori, Siaya, Busia, Bungoma, Vihiga na Kakamega.