Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR na harakati za kuhamisha wakimbizi walio hatarini  kutoka Libya

Afisa wa IOM akikagua nyaraka za wahamiaji kutoka Nigeria kabla ya kupanda Basi kurejea kwao wakitokea Libya.
IOM/Marian Khokhar
Afisa wa IOM akikagua nyaraka za wahamiaji kutoka Nigeria kabla ya kupanda Basi kurejea kwao wakitokea Libya.

UNHCR na harakati za kuhamisha wakimbizi walio hatarini  kutoka Libya

Wahamiaji na Wakimbizi

Wakimbizi 98 wamesafirishwa kutoka Libya kuelekea Italia Alhamisi ikiwa ni zoezi la tatu kutoka nchi hiyo mwaka huu.

Wakati Libya ikiendelea kukabiliwa na mzozo, usafirishaji wa wahamiaji ni muhimu ili kuokoa maisha ya wengi wao wanaoishi vizuizini na maeneo ya mjini ambao wako hatarini huku wakihitaji usalama na ulinzi.

Wakimbizi hao ni kutoka Eritrea, Ethiopia, Somalia na Sudan ikiwemo watoto 52 ambao wamesafiri bila mzazi au mlezi. Mtoto mchanga kabisa ni Yousef, mweny umri wa miezi saba kutoka Somalia aliyezaliwa kizuizini wakati akisafiri na wazazi wake. Wengi wa wakimbizi walikuwa wameshikiliwa vizuizini kwa muda mrefu, wengine zaidi ya miezi nane. Mkimbizi huyu kutoka Eritrea ni miongoni mwao, “Jina langu ni Nagaste, nimetokea Eritrea miaka miwili iliyopita. Sasa nimefurahi sana kwamba naelekea Italia. Nilikuwa katika kizuizi cha Azzawya. Sasa ni mazingira bora kwenye kizuizi na watu kutoka pale kizuizini wanakuja pia. Mungu awabariki. Ninafuraha sana. Siamini kwamba naenda Italia.”

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linatoa shukrani zake kwa ushirikiano na wizara ya Libya ya mambo ya ndani na kwa msaada kutoka kwa wadua LibAid kwa msaada wao kuhakikisha kuachiwa na kusafirishwa kutoka kwa vizuizi. Paula Barrachina msemaji wa UNHCR nchini Libya anasema, “leo UNHCR inahamisha wakimbizi 98 walioko hatarini kutoka Libya. Kuhamishwa kwa wakimbizi ni kuokoa Maisha yao, na kuwapa mustakabali wenye matumaini kwa wakimbizi wengi a,bao walikuwa wamezuiliwa nchini Libya kwa kipindi cha miezi nane. Tunaendelea kutoa wtio kwa jamii ya kimatifa kuendelea kutoa fursa nyingi za kuhamisha na kuhifadhi wakimbizi waliohatarini kutoka Libya na tunamatumaini kwamba tunaweza kuendelea na program hii ya kuokoa Maisha na kusaidi wakimbiai wengi waliokwamba Libya.”

UNHCR kufikia sasa imesaidia wakimbizi 1,474 walio hatarini kutoka Libya mwaka huu wa 2019 ikiwemo kusafirisha wakimbizi 710 kwenda Niger, 393 Italia, 371 wamepta hifadhi nchi za Ulaya na Canada.

Akikaribisha makubalianao ya wiki hii ya Muungano wa Afrika na Rwanda kuunda kituo cha mpito kwa ajili ya kuwaokoa wakimbizi walioko hatarini kutoka Libya, kamishan mkuu wa UNHCR ametoa wito kwa nchi zingine kuiga mfano huo na kuchukua hatua kuokoa maisha.