Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa na Benki ya dunia watoa wito wa misaada kuinusuru Somalia

Maisha nchini Somalia kwa muda mrefu yamekuwa magumu kutokana na vita isiyokoma.
OCHA/Cecilia Attefors
Maisha nchini Somalia kwa muda mrefu yamekuwa magumu kutokana na vita isiyokoma.

Umoja wa Mataifa na Benki ya dunia watoa wito wa misaada kuinusuru Somalia

Msaada wa Kibinadamu

Pamoja na uchambuzi wa hivi karibuni unaoonyesha kuwa mavuno ya Somali yalikuwa mabaya zaidi tangu janga la njaa mnamo mwaka wa 2011, Mkuu wa misaada ya dharura kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Mark Lowcock, leo ametoa wito wa msaada wa fecha ulio endelevu kwa ajili ya kulinda mazao yaliyopatikana hivi karibuni kwa lengo la kudhibiti njaa.

Bwana Lowcock ameyasema hayo akizungumza mwishoni mwa ziara yake ya siku mbili nchini Somalia aliyoambatana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa  ajili ya ajenda ya Maendeleo ya 2030, Mahusiano ya Umoja wa Mataifa, na Ushirikiano, Mahmoud Mohieldin, na Katibu mkuu msaidizi wa Umoja wa Mataifa wa msaada wa Ujenzi wa amani, Oscar Fernandez-Taranco.

"Mchanganuo wa hivi karibuni wa uhakika wa chakula huko Somalia unaonyesha kuwa juhudi zetu zinafanikiwa. Takriban Wasomali milioni moja wanakabiliwa na njaa leo ikiwa ni idadi ndogo kuliko ilivyodhaniwa kwa sababu tulichukua hatua mapema tulipoona hali inaweza kuzorota zaidi na kwa sababu wafanyikazi wa misaada wanatekeleza wajibu wao kama inavyohitajika, "amesema Bwana Lowcock.

Pamoja na migogoro inayoendelea,changamoto hizi zinaendelea kuwafurusha watu kutoka makwao. Watu milioni 2.6 waliohamishwa makazi yao mara nyingi hubaguliwa kwenye mipaka ya jamii, wanakabiliwa na kufukuzwa na ufidhuli mwingine.

Ujumbe huo ulitembelea Baidoa ambako takriban watu 360,000 waliokimbia ukame, shambulio la kigaidi na vita kwa miaka mitatu iliyopita wanaishi katika makazi 400 ndani na karibu na mji huo.

Katika mkutano na Waziri Mkuu Hassan Ali Khaire kule Baidoa, viongozi hao watatu waliipongeza Serikali kwa uongozi wake na kusisitiza kujitolea kwao kuunga mkono Serikali kushughulikia athari za janga la njaa kutorudia.

"Benki ya Dunia itaendelea kuunga mkono juhudi za Somalia za kuongeza uwekezaji katika sekta na miundombinu ya uzalishaji sambamba na vipaumbele vya mfumo wa Urejesheaji amani na mpango mpya wa Maendeleo wa Kitaifa wa mwaka 2020-2024," amesema Bwana Mohieldin. "Walakini, kupata uwekezaji mkubwa wa ziada kunahitaji Somalia kuukabili mpango wa nchi maskini yenye madeni. Kwa hivyo, miezi ijayo itakuwa muhimu na tunakaribisha juhudi za mamlaka ya kudumisha rekodi nzuri iliyoanzishwa miaka michache iliyopita juu ya mageuzi ya utawala wa kitaifa. "

Kwa pande wake Lowcock amesema"Kufuatia kutopata mavuno na athari za mafuriko, nawasihi wafadhili kuongeza msaada wao kwa ukarimu ili kuwezesha utoaji wa msaada wa kuokoa maisha pamoja na suluhisho la muda mrefu katika kusaidia kuzuia kutokea tena kwa majanga ya kibinadamu,"