Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ITU na Cisco wazindua mradi wa kuimarisha stadi za kidijitali

Vijana wakitumia kompyuta mjini Kampala, Uganda.
World Bank/Arne Hoel
Vijana wakitumia kompyuta mjini Kampala, Uganda.

ITU na Cisco wazindua mradi wa kuimarisha stadi za kidijitali

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Shirika la muungano wa mawasiliano duniani ITU, kwa kushirikiana na Cisco, kampuni inayohusika na bidhaa za intaneti, leo wamezindua vituo vya kutoa mafunzo ya kidijitali kwa ajili ya kuwapatia watu stadi zinazohitajika kushiriki katika jamii ya zama za sasa za kidijitali na uchumi.​​​​​

Kupitia mradi huo uliozinduliwa kwenye ofisi za ITU, washirika hao wawili watafanya kazi na mtandao wa taasisi kwa ajili ya kuendesha programu katika maeneo maalum ya kiteknolojia.

Taarifa ya pamoja ya ITU na Cisco iliyotolewa Budapest Hungary imesema kutoa mafunzo ya stadi za kidijitali ni muhimu katika kuziba pengo la kidijitali kwani stadi hizo zinahitajika katika viwango tofauti, katika viwango vya msingi kwa ajili ya kusaidia watu kuwasiliana na kunufaika na huduma za intaneti na kiwango cha pili kusaidia wanafunzi na wasaka ajira kupata stadi zinazohitajika katika uchumi wa kidijitali na kiwango kilichoendelea kwa ajili ya kuongeza wataalam wa teknolojia ya habari na mawasiliano na kuweza kukabiliana na mahitaji ya sekta hiyo.

Mradi huo unalenga watu ambao wanahitaji stadi za msingi za kidijitali kwa ajili ya kutumia vifaa hivyo kufikia huduma kupitia mtandao na wale wanaolenga kuimarisha stadi zao kuwa kiwango cha pili. Mradi unalenga pia wafanyabiashara ambao wanalenga kuimarisha biashara zao na inasaidia watunga será katika kubuni na kutekeleza sera na programmu ambazo zinaendana na stadi za kidijitali kwa lengo la kuwezesha mchakato bunifu w akidijitali.

Mradi utategemea ushirikiano wa wadau mbalimbali ambapo katibu mkuu wa ITU, Houlin Zhao amesema, “tunafuraha kuungana na Cisco kuimairsha uelewa wa kidijitali, tunatoa wito kwa serikal, sekta binafsi, mashirika ya maendeleo na jamii za mashinani na wadau wengine kutusaidia kuendeleza mradi. Kuunganan nasi kuimarisha stadi za kidijitali na kuwezesha mabadiliko ya kidijitali na kuongeza kasi kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa.”

Kwa upande wake Laura Quintana, naibu rais na mkurugenzi mkuu wa chuo cha Cisco cha kujenga mahusiano amesema, “tunafurahi kushirikiana na ITU katika vituo vya kubadili mienendo ya kidijitali ambayo itasaidia chuo kuandaa watu binafsi na stadi katika teknolojia pamoja na maeneo ya uwekezaji ambako mafunzo kupitia mradi ni muhimu.”

Katika kuanzisha mradi, ITU na Cisco itatambua vituo kumi ambavyo vitashirika awamu ya kwanza ya miezi 18 kuanzia Januari 2020. Vituo hivo vitakuwa Marekani na Amerika Kusini, Afrika na maeneo ya Asia Pasifiki.