Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirika wa Kusini-Kusini ni mfano wa kuigwa:Guterres 

Wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa wakati wa kufunga pazia mkutano wa ngazi ya juu wa pili kuhusu ushirikiano wa kusini-kusini uliofanyika Buenos Aires, Argentina.
UNOSSC/Rodrigo Atanes
Wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa wakati wa kufunga pazia mkutano wa ngazi ya juu wa pili kuhusu ushirikiano wa kusini-kusini uliofanyika Buenos Aires, Argentina.

Ushirika wa Kusini-Kusini ni mfano wa kuigwa:Guterres 

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema miongo ya hivi karibuni imeonyesha nguvu ya Ushirika wa Kusini-Kusini katika kusongesha mbele malengo ya maendeleo endelevu au SDGs.

Katika ujumbe wake maalumu kwa ajili ya siku ya kimataifa ya ushirika wa Kusini-Kusini Antonio Guterres amesema mataifa yanayoendelea, watoto zaidi wanahudhuria shule, ukilinganisha na kwingineko, pia viwango vya vifo vya watoto na kina mama vimepunguzwa kwa karibu nusu, na umaskini uliokithiri umepunguzwa sana.

Ameongeza kuwa kwa, kuongozwa na ari ya mshikamano, kuheshimu uhuru wa kitaifa na ushirikiano ulio sawia, Ushirika wa Kusini Kusini umetoa suluhisho kamili kwa changamoto za pamoja, huku nchi nyingi zikiwa vyanzo vya msaada kwa mataifa mengine na msukumo wa njia za maendeleo zilizo bunifu.

Guterres amesema lakini mzigo mkubwa wa umaskini unabaki kwenye nchi zinazoendelea za kusini, na hata katika nchi zenye uchumi unaokua haraka. Maendeleo hayana kasi ya kutosha kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu mnamo mwaka 2030, na huku akisistiza kwamba mafanikio yanastahili kugawanywa kwa uwiano zaidi.

Amesema kana kwamba hiyo haitoshi , dharura ya mabadiliko ya tabianchi inatishia hatua kubwa iliyopigwa kwa miongo kadhaa. “Kwa kweli, Nchi zinazoendelea tayari zimeathiriwa sana na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi.”

Hata hivyo amesisitiza kwamba ushirika wa Kusini Kusini hauwezi kuwa mbadala wa  usaidizi rasmi wa maendeleo au kuchukua nafasi ya majukumu ya nchi zilizoendelea yaliyowekwa bayana katika Ajenda ya hatua ya Addis Ababa na Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris.

Ila Ushirika huo wa Kusini Kusini unaendelea kuwa mfano wa katika kasi ya maendeleo ambayo hayamwachi mtu yeyote nyuma. Ili kuongeza uwezo huo, amesema “lazima tuunganishe juhudi hizi na tuweke mikakati endelevu ya kuleta tija na kwamba katika Siku hii ya Kimataifa, “turejee ahadi yetu ya kufikia Agenda ya 2030 kwa kujifunza kutokaushirika ulioboreshwa wa Kusini Kusini.”

Siku ya kimataifa ya ushirika wa Kusini Kusini huadhimishwa kila mwaka Septemba 12.