Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila kubadili mwelekeo hatua zilizopigwa katika SDG’s ziko hatarini:UN

Mwanamke nchini Afghanistan akiwa amesismama pembeni ya mtambo wa nishati ya jua au Sola wa kupikia
UNDP/Rob Few
Mwanamke nchini Afghanistan akiwa amesismama pembeni ya mtambo wa nishati ya jua au Sola wa kupikia

Bila kubadili mwelekeo hatua zilizopigwa katika SDG’s ziko hatarini:UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Mfumo wa sasa wa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG’s unatishia kurudisha nyuma hatua kubwa zilizopigwa katika mchakato huo endapo hatutafanyika mkakati madhubuti wa kubadili mwelekeo limesema kundi la wanasayansi huru lililokamisha uzinduzi wa ripoti yake mpya hii leo Jumatano.

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa ndiyo itakuwa kitovu cha majadiliano ya mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhudu SDG’s utakaofanyika baadaye mwezi huu.Hali mbaya ya kutokuwepo usawa na uwezekano wa athari ambazo hazitoiweza kubadilishwa katika mazingira ambayo wote tunayategemeea , inahitaji kuchukuliwa hatua muafaka, imesema idara ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kiuchumi na kijamii (DESA), katika taarifa yake kuhusu matokeo ya ripoti hiyo iliyoandaliwa na timu ya wataalam 15 walioteuliwa na Umoja wa Mataifa.

Katika ripoti hiyo wataalam hao wamesema “Kufukia mustakabali bota kwa wote na kutokomeza kabisa umasikini kwa watu wote duniani wanaotarajiwa kufikia bilioni 8.5 ifikapo mwaka 2030 bado inawezekana, lakini tu endapo kutakuwa na mabadiliko ya msingi nay a haraka katika uhusiano baina ya watu na mazingira ya asili.”

Ripoti hiyo “Mustakabali ni sasa:sayansi kwa ajili ya kutimiza malengo ya maendeleo endelevu “ inaainisha uelewa wa uhusiano baina ya malengo ya SDGs na mfumo ambao unaielezea jamii ya sasa, ili kuwa na mpango ambao utarehesha utulivu wa maendeleo duniani.

Kwa maombi ya nchi wanachama kutathimini mchakato wa hatua zilizopigwa kuhusu ajenda yam waka 2030 ya SDGs iliyopitishwa mwaka 2015 , ripoti hiyo ya kimataifa kuhusu maendeleo endelevu (GDSR) imejumuisha utafiti wa kisayansi kutoka kwenye maisha ya baharini, hadi matumizi endelevu, uzalishaji na udhibiti wa majanga miongoni mwa masuala .

Mapendekezo yanayoungwa mkono na sayansi

Mchakato wa sasa wa maendeleo umeleta matunaini na nuru kwa mamilioni ya, kwa mujibu wa matokeo ya kisayansi , lakini gharama ya rasilimali nyingine na kuongezeka kwa kutokuwepo usawa ambako kunaathiri ukuaji wa kimataifa.

Ripoti inasema kupiga jeki uchumi kwa kuongeza matumizi kwa mfano kunachosha rasilimali za dunia na kutengeneza sumu za bidhaa hizo ambazo ni tishio kubwa kwa dunia. Katika kiwango cha sasa cha matumizi “Utumiaji wa malighafi unatarajiwa kuongezeka mara mbili kati ya mwaka 2017 na 2060kutoka gigatani 89 hadi gigatani 167 na kusababisha athari kubwa ikiwemo za ongezeko la gesi ya viwandani na athari za sumu zingine kutokana na rasilimali ambazo zimetumiwa kupita kiasi.”

Wanasayansi hao wamesisitiza ni lazima mfumo ubadilike ili kuepuka hasara zaidi katika mahusiano ya kijamii na ukuaji endelevu wa uchumi, kukabiliana na kupotea kwa bayoanuai na kuinusuru dunia inayoelekea ukingoni na kutokana na mfumo wa taibanchi duniani.

Ili haya yafanikiwe ni lazima sekta zote zishikamane kuchukua hatua zilizoratibiwa pamoja limesema kundi hilo la wanasayansi, na kuongeza uwekezaji wa kisayansi kwa ajili ya uendelevu ni mtazamo mmoja muhimu, na kutambua kwamba utimizaji wa SDGs unahitaji ukuaji wa kiuchumi kupewa msukumo kutoka katika uharibifu wa mazingita huku pia likipunguzwa pengo la kutokuwepo usawa.

Hata hivyo wanasayansi hao wamesema wanatambua kwamba mabadiliko makubwa kabisa yanayohitajika hayatakuwa kazi rahisi na ripoti yao inapendekeza kwamba uelewa mkubwa wa kisayansi unahitajika ili kung’amua na kudhibiti shinikizo na na mambo kwenda mrama katika kubadili mfumo.

Masuala muhimu ya kuyafanyia kazi

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kuna masuala 20 ya kuingilia kati ambayo yanaweza kutumika kuchagiza haraka mchakato wa utekelezaji wa malengo katika miaka 10 ijayo.

Miongoni mwa mambo hayo 20 ni huduma za msingizinapaswa kuhakikisha zinapatika duniani kote zikiwemo za afya, elimu, maji na usafi, miundombinu, nyumba na ulinzi wa hifadhi ya jamii, kama chachu ya kuelekea kutokomeza kabisa umasikini.

Zaidi ya hayo ni kukomesha ubaguzi wa kijamii na kisheria, kuongeza vyama vya ushirika wa kibiashara, mashirika yasiyo ya kiserikali, makundi ya wanawake na jamii zingine kwa ujumla zitakuwa mdau muhimu katika juhudi za utekelezaji wa ajenda ya mwaka 2030.

Ripoti kamili na mapendekezo yake itawasilishwa wakati wa kongamano la ngazi ya juu la kisiasa la mwaka 2019 kuhusu SDGs ambalo litajumuisha wakuu wa nchi na serikali mjini New York Marekani hapo 24 na 25 Septemba.