Wanahabari wana wajibu mkubwa katika kurejesha amani Mashariki ya Kati: Katibu Mkuu

11 Septemba 2019

Wandishi wa habari ni wadau muhimu katika mchakato wa kurejesha amani katika ukanda wa Mashariki ya Kati ambako mzozo umesambaratisha uchumi na harakati za kibinadamu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataiaf, Antonio Guterres.

Guterres amesema haya kupitia ujumbe wake kwa mkutano wa kimataifa wa wanahabari kuhusu juhudi za kurejesha amani katika ukanda wa Mashariki ya Kati amabo umeong’oa nanga hii leo mjini Ankara, Uturuki.

Katika mkutano huo wa Umoja wa Mataifa mwaka 2019, Bwana Guterres amesema si msaada wa kibinadamu wala kiuchumi unaoweza kusuluhisha mzozo Mashariki ya kati bali dhamira ya jamii ya kimataifa na wadau wote.

Amesema kwa sasa mgogoro wa kisiasa, kiuchumi na kibinadamu unaondelea katika eno la Kipalestina linalokakaliwa umefikia kiwango cha juu zaidi. Na kuongeza kwamba kwa bahati mbaya katika mwaka uliopita, hatua zilizopigwa zimeenda mrama na malengo huku hali ya usalama ikizorota na kuendelea kudhili watu wa Palestina na Israel.

Amerejelea tamko lake kwamba amani yaweza kupatikana kupitia kufufuliwa kwa kwa maono ya mataifa mawili, Israel na Palestina, kila moja kivyake kwa amani na usalama.

Hali katika ukanda wa Gaza inasikitisha kulikomengine kwani watu takriban  milioni mbili wa Kipalestina wakisalia katika kimbiakimbia, kuzuiliwa kufikia sehemu fulani, wakiishi katika umaskini unaoongezeka na uhaba wa ajira na kutofikia huduma za afya maji na umeme vipasavyo.

Bwana Guteres amesema nilazima jamii ya kimataifa ichuke hatua za dharura na dhamira ili kuhsughulikia mahitaji ya kiuchumi na kibinadamu ya Wapalestina.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud