Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinazoendelea lazima zibadili mwelekeo kuacha utegemezi wa bidhaa:UNCTAD

Mukhisa Kituyi, Katibu Mtendaji wa Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD wakati wa mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.
UNnewskiswahili/Patrick Newman
Mukhisa Kituyi, Katibu Mtendaji wa Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD wakati wa mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.

Nchi zinazoendelea lazima zibadili mwelekeo kuacha utegemezi wa bidhaa:UNCTAD

Ukuaji wa Kiuchumi

Mabadiliko katika uzalishaji wa bidhaa ndiyo njia bora ya kukabiliana na changamoto zinazotokana na na mabadilliko ya tabia nchi kwenye nchi zinazoendelea  kwa mujibu wa ripoti ya  Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Matafa UNCTAD. Jason Nyakundi anatupasha zaidi

Mabadiko hayo yatahusu uzalishaji wa bidhaa mpya na pia sekta zingine ili kupunguza utegemezi wa bidhaa moja.

 Janga na mazingira limekuwa hatari kubwa kwa nchi zinazotegemea bidhaa moja na itasababisha kuporomoka kwa baadhi ya chumi ikiwa hatua hazitachukuliwa sasa, alisema katibu mkuu wa UNCTAD Mukhisa Kituyi.

Kutokana na kuwa nchi zinazotegemea bidha huchangia kwa kiwango kikubwa  katika maadiliko ya tabia nchi, hali hiyo huziweka katika hatari kubwa.  Na kuongeza kwamba

(SAUTI YA MUKHISA KITUYI)

Changamoto za nchi zinazotegemea bidhaa imekuwa nasi kwa muda mrefu, katika majadaliano kwa muongo mmoja tumeshuhudia kwamba katika muongo uliopita wa karne hii kulikuwa na mlipuko wa bidhaa na ambapo ungetarajia kwamba serikali zingewekeza katika miundombinu, katika kuimarisha stadi za watu na kusambaza vitega uchumi tulichokishuhudia tu ni ongezeko la miradi ya hadhi na matumizi ya juu na wakati mnyororo ulilipuka tumeshuhudia ongezeko la deni la nchi na kusambaratika kwa miundombinu iliyokuwa imeasisiwa wakati wa mlipuko na kutopanua wigo wa uwekezaji katika chumi nyingi

Pia amesema nchi hizo ziko kwenye hatari kwa kuwa hutegemea sana katika sekta ambazo huathiriwa na majanga ya kimazingira. Nchi ndogo za visiwani zikiwa ndizo huathiriwa  zaidi.

 Kupanda kwa joto la bahari huwa hatarari kubwa kwa nchi za visiwa ambazo uchumi wai hutegemea sekta ya uvuvi kama vile nchi ya Kiribati kwa asiliami 88 kati ya mwaka 2013-2017, Maldives asilimia 79 na visiwa vya Micronesia kwa asilimia 75.

 Athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa uzalishaji wa mimea na samaki ni mkubwa katika sehemu za nyanda za chini ambapo nyingi ya nchi hizo zipo.

Pia zilizo kwenye hata ri ni nchi zinazotemea mafuta na gesi kama vile Brunei, Darussalam, Kuwait na Qatar zilizo na uzalishaji  mkubwa zaidi viwango vya juu vya gesi chafu.

 Ripoti hiyo inasema kuwa nchi hizio zinastahili kuachana na utegemezi kwa bidhaa moja. Pia ni lazima zichukue hatua  na kukabilina na  mabadiliko ya tabia nchi zilnazochukuliwa na nchi zingine, ambazo zinatajarajiwa kupunguza mahitaji ya bidhaa muhumi ambazo nchi hizo hutegemea.

 Fursa na changamoto

Hatua za kukabiliana na mabadilia ya tabia nchi nazo zina fursa kwa nchi zinazoendelea zinazotegemea bidhaa moja kulingana na ripoti.

Inasema kuwa harakati  za dunia nzima za kuelekea katika matumizi ya nishati safi ni fursa kubwa kwa nchi zilizo la mali ghafi ya bidhaa zinazotumiwa kwenye nishati safi kama vile betri za nishati ya jua, nishati ya upepo na betri za magari yanayotumia umeme.

Kwa mfano mwaka 2018 Jamhuri ya Demokasri ya Congo ilichangia uzalishaji wa asilimai 58 ya madini ya Cobalt ambayo ni bidhaa muhimu inayotumiwa katika betri za magari yanayotumia umeme, huku Chile na Argentina zikichukua asilimia 71 yamadini ya Lithium, bidhaa muhimu katika kutengeza betri.