Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waafghanistan wote wanapaswa kuunga mkono mazungumzo ya amani:Yamamoto

Maadhimisho ya miaka 100 ya Uhuru wa afghanistan yalisherehekewa kwenye mji wa Kandahar mwezi agosti 2019 kwa mamia ya watu kuandamana na bendera za taifa lao mitaani
UNAMA / Mujeeb Rahman
Maadhimisho ya miaka 100 ya Uhuru wa afghanistan yalisherehekewa kwenye mji wa Kandahar mwezi agosti 2019 kwa mamia ya watu kuandamana na bendera za taifa lao mitaani

Waafghanistan wote wanapaswa kuunga mkono mazungumzo ya amani:Yamamoto

Amani na Usalama

Mgogoro wa miaka nenda miaka rudi wa Afghanistan unaweza kutatuliwa tu kwa njia ya mazungumzo ya amani kati ya makundi ya watu w anchi hiyo amesema mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA.

Tadamichi Yamamoto ambaye pia ni mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan ameyasema hayo mbele ya kikao maalum cha Baraza la usalama akisistiza kwamba na mazungumzo hayo ni lazima yake jumuishi na yanayowakilisha jamii nzima ya Afghanistan.

Ameongeza kuwa “Matukio ya siku na wiki za hivi karibuni yameonyesha sasa kuluko wakati mwingine wowote haja ya haraka ya kusaka suluhu ya kisiasa kwa mgogoro wa muda mrefu wa Afghanistan.Juhudi za amani za mwaka uliopita zimeleta matumaini, lakini pia hofu kwa walio wengi.”

A,esema “Wanatumai kumalizika kwa vita lakini pia wanahofia amani hiyo huenda ikaja kwa kuweka rehani uhuru na haki vitu ambavyo taifa hilo limekuwa likijaribu kuvilinda kwa takribani miaka 18 iliyopita. Wasichana wanahofia hapo siku za baadaye ushiriki wao katika masuala ya kijamii , kiuchumi na maisha ya kisiasa nchini mwao.”

Bwana Yamamoto ameliambia Baraza la Usalama kwamba “muafaka wowote wa kiasiasa lazima ujumuishe ahadi ya kulinda na kusongesha mbele haki za binadamu na uhuru kwa watu wote wanaoishi Afghanistan, ikiwemo wanawake, vijana, na walio wachache lakini pia uhuru wa kujieleza na wa vyombo vya Habari.”

Baraza limekutana leo siku chache tuu baada ya mazungumzo ya ana kwa ana ya miezi kadhaa baina ya kundi la Taliban lenye itikadi Kali ambalo lilikuwa linaidhibiti nchini huyo tangu uvamizi wa ushirika wa 2001 ambao umetangazwa na Rais wa Marekani Dolnald Trup kuwa umekufa.

Tadamichi Yamamoto, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan na mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMA, akitoa taarifa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali nchini Afghanistan na athari zake kwa amani na us
UN Photo/Loey Felipe
Tadamichi Yamamoto, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan na mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMA, akitoa taarifa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali nchini Afghanistan na athari zake kwa amani na us

Pande hizo mbili ziliarifiwa kuwa zilikaribia kufikia muafaka na kukamilisha makubaliano ya amani ambayo hayakuhusisha serikali ya Afghanistan ambayo inatambulika kimataifa.

Mkuu huyo wa UNAMA  amewaambia wajumbe wa Baraza kwamba mafanikio mengine makubwa yaliyopatikana katika miaka 18 iliyopita ambayo yanahitaji kudumishwa na kuchagizwa ni uwezo wa taasisi za serikali. Amehimiza kuwa “ili kusonga mbele juhudi za amani zinahitaji kushughulikia na kupunguza machafuko na kusitisha uhasama, na msaada wa kikanda ni muhimu sana.”

Uchaguzi kufanyika baadaye mwaka huu

Raia wa afghanistan watafanya uchaguzi mkuu tarehe28 Septembea mwaka huu, uchaguzi ambao utakuwa ni wa nne wa rais tangu mwaka 2001. “Uchaguzi huru na wa kuaminika utaweka msingi imara na muhimu wa kisiasa kwa ajili ya mustakabali wa nchi hiyo pamoja na uhalali na mamlaka kwa Rais atakayechaguliwa.Na hii itakuwa muhimu sana kwa mchakato wa amani.”

Mchango wa ofisi zingine za UN

Bwana Yamamoto ameongeza kuwa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa na uhalifu UNODC inaisaidia Afghanistan katika kusaka njia bora inayozingatia afya katika usambazaji wa mihadarati na inavyohitajika.

Timu inayokwenda sehemu mbalimbali na kitengo cha kudhibiti mihadarati wamefanikiwa kukamata kilo 800 za heroin, zaidi ya tani 1.2 ya afyunyi, karibu tani tisa za Hashis na zaidi ya lita 7,500 za kemikali ambayo inatosheleza kutengezeza zaidi ta tani tatu za heroin.

Mkuu wa UNODC Yury Fedotov amekaribisha azma ya Afghanistan ya kukomesha mashambulizi na ameipongeza serikali ya nchi hiyo kwa kuanzisha na kushirikiana uqwenyekiti mwenza na Hispania katika kundi la marafiki wa wahanga wa ugaidi.