Masharti ya taasisi za kifedha yana mchango katika kukandamiza haki za binadamu-Mtaalamu wa UN

10 Septemba 2019

Masharti ya maadili yanayowekwa na taasisi za kimataifa za kifedha kama vile shirika la fedha duniani  IMF, mara kwa mara yanasababisha ukikukwaji wa haki za binadamu, amesema mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu madeni ya nje na haki haki za binadamu Bwana Juan Pablo Bohoslavsky katika ripoti yake itakayowasilishwa kwa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Oktoba.

Akiongea hii leo mjini Geneva Uswisi, Bwana Bohoslavsky amesema,“Ingawa masharti yanaweza kuwa njia ya udhibiti dhidi ya matumizi mabaya ya rasilimali, ni muhimu kukumbuka kuwa masharti ya uadilifu  yanathiri makundi  tofauti katika jamiii na kwa namna tofauti hususani wale walioko hatarini na pia waliotengwa.”

Pia ameongeza kuwa, “ingawa mataifa ndio dhamana kuu ya haki za binadamu, taasisi za kifedha za kimataifa zinaweza kuwajibika ikiwa wataweka sera ambazo zina matokeo mabaya kwa haki za binadamu.”

UN Photo/Jean-Marc Ferré
Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu madeni ya nje na haki haki za binadamu Bwana Juan Pablo Bohoslavsky

 

Bwana Bohoslavsky anahoji, “kama taasisi za kimataifa za fedha zinaweza kuwajibishwa kwa madhara yanayozuilika yaliyosababishwa na bwawa lilijengwa kwa ufadhili wao, kwa nini wasiwajibike kwa madhara yanayozuilika dhidi ya haki za binadamu yaliyotokana na sera mbaya za kiuchumi?.”

Sheria ya kimataifa ya haki za binadamu inazuia nchi kulazimishwa kulipa madeni yake yote kwa ukamilifu kwa gharama ya kuongezeka kwa vifo vya wa watoto, ukosefu wa ajira na utapiamlo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud