Vita vilitutenga, lakini tunachopigania ni elimu:mabinamu wakimbizi toka CAR

10 Septemba 2019

Hakuna kitu kibaya duniani kama vita, kwani vinasambaratisha familia, nchi hata ndoto, kwa majubu wa mabinamu wawili kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR waliolazimika kufungasha virago na kukimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013.

Kijijini Mongoumba nchini CAR ambako mabinamu Prince-Bonheur Ngoungou na Gothier Semi walilazimika kuvuka mto mto ubangi kukimbia vita wanasema watoto wengi walipoteza elimu na kwa miaka mitano hawakuweza kuhudhuria masomo wakiwa ukimbizini hali ambayo ilikuwa ngumu sana kwani ndoto zao waliziona shuleni.  Kwa miaka hiyo mitano wakitenganishwa na mto Prince alieshia Congo Brazzaville na Ghothier Semi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

(SAUTI YA PRINCE -BONHEUR NGONGOU)

« tangu nilipoondoka sikuweza kwenda shule  nilikaa bure tu bila kusoma »

Kwa upande wake Ghothier

(SAUTI YA GOTHIER SEMI)

“kupoteza miaka mitano ya masomo imenirudisha nyuma sana”

Tangu 2016 amani imeenza kurejea taratibu CAR na mwa msaada wa shirika la wakimbizi UNHCR Gothier alirejea nyumbanina sasa karudi tena shuleni

(SAUTI YA GOTHIER -CUT 2)

“Elimu ni ufunguo wa maisha bila elimu siwezi kuishi kwa amani”

Kwa bahati mbaya binamu yake Prince bado yuko ukimbizini upande wa pili wa mto n ani miongoni mwa wakimbizi 30,000 wanaosubiri kurejea nyumbani.

(SAUTI YA PRINCE CUT 2)

“Maisha bila shule sio Maisha , shule ndio mustakabali wangu”

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud