Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

PAHO yatoa ombi la msaada wa dola milioni 3.5 kwa huduma za kibidamu Bahamas

Muonekano wa juu wa visiwa vya Bahama kufuatia kimbunga Dorrain ambako wadau mbali mbali wanatoa msaada.
U.S. Coast Guard District 7
Muonekano wa juu wa visiwa vya Bahama kufuatia kimbunga Dorrain ambako wadau mbali mbali wanatoa msaada.

PAHO yatoa ombi la msaada wa dola milioni 3.5 kwa huduma za kibidamu Bahamas

Msaada wa Kibinadamu

Muungano wa shirika la afya la nchi za Amerika (PAHO) na lile na Afya duniani (WHO) umetoa ombi la dola milioni 3.5 kwa wafadhili ili kugharamia kipindi kifupi cha huduma  za afya na mahitaji mengine kwa watu walioathiriwa na kimbunga Dorian huko Bahamas.

Kimbunga hicho cha kiwango cha daraja la tano kilichosababisha uharibifu mkubwa kilitua wiki moja iliyopita kaskazini magharibi mwa Bahamas na kuathiri vibaya sekta ya afya huku kikiharibu vifaa na miundombonu ya umeme na maji.

Takriban watu 73,000 wameathiriwa na kibunga hicho na kuna mamia ya wengine walioa kwenye makao katika maeneo yaliyoathiriwa. Huku vifo 43 vikiwa vimeripotiwa hadi sasa, idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka wakati maeneo zaidi yanafikiwa na shughuli za kutafuta na kuokoa zikiendelea.

Mmoja wa manusura wa kimbunga Dorian Bwana Charles Cornish kutoka mji wa Spring City, Abaco anasema walipambana usiku kucha kujikoa, na anaamini bado kuna watu bado wamekwama, anasema, "unajua, hivi sasa kuna watu wengi huko…huko siyo mahali pa mtu kuwepo hivi sasa hadi pale ambapo serikali itapata namna ya kusafisha eneo lote.”

Dr. Ciro Ugarte, mkurugenzi wa huduma za dharura katika PAHO alisema, lengo letu kurejesha hudumua muhimu za afya, kuhakikisha uwepo wa maji katika maeneo yaliyoathiriwa na vituo vya afya na pia kurejesha huduma zingine za usafi.

Dola 3.5 zinazoitishwa na  PAHO/WHO ni makadirio tu ya kugharamia huduma za muda mfupi za afya, maji na usafi katika visiwa vya Bahamas vilivyoathiriwa  zaidi na kimbunga Dorian katika kipindi cha miezi sita inayokuja.