Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UN na wadau waendelea na harakati za kutoa msaada Bahamas

Madhara kutokana na kimbunga Dorrain ni dhahiri eneo la Treasure Cay, Bahamas walinda bahari kutoka Marekani wanashirikiana na vikosi Bahama katika kutafuta na kuokoa watu.
U.S. Coast Guard District 7
Madhara kutokana na kimbunga Dorrain ni dhahiri eneo la Treasure Cay, Bahamas walinda bahari kutoka Marekani wanashirikiana na vikosi Bahama katika kutafuta na kuokoa watu.

Mashirika ya UN na wadau waendelea na harakati za kutoa msaada Bahamas

Msaada wa Kibinadamu

Wakati Umoja wa Mataifa na watoa misaada wengine wakiendelea na shughuli za kutoka msaada katika visiwa vya Bahamas ripoti za hivi punde zinaashiria kwamba idadi ya vifo huenda ikaongezeka kwa mujibu wa Shirika la afya ulimwenguni, WHO.

Akizungumza na waandishi wa habai mjini Geneva, Uswisi mkurugenzi wa timu za tiba ya dharura kwenye WHO, Ian Norton  amewaambia waandishi wa habari kwamba idadi inatarajiwa kuoongezeka ijapokuwa hawezi kusema idadi lakini kwamba wana wasiwasi kuhusu hilo akiongeza kwamba

(Sauti ya Ian)

“Kile tunachoona, na kile ambacho tumeshaona kwa bahati mbaya katika kimbunga hiki ni kile unachoona pengine baada ya tsunami. Na kile tusichoona ni yale majeraha; tunaona watu wengi wamezama na kupoteza maisha yao au wakiwa wamenusurika.”

Kufikia sasa watu 30 wamethibitishwa kufariki kufuati kimbunga Dorian kupiga visiwa vya Abaco na Grand Bahama mwisho wa wiki iliyopita kwa upepo wa kasi ya kilometa 297 kwa saa

Kwa mujibu wa serikali, maelfu ya watu bado hawajulikani waliko kufuatia kimbunga hicho cha kiwango cha tano na urefu wa mita 5.5 hadi 7 na watu 76,000 wanakadiriwa kupoteza makazi yao.

Dkt. Norton amesema kwas asa mahitaji ya dharura ni pamoja na kutibu watu walio na magonjwa ya muda mrefu kwa mfano walio na kisukari au magonjwa ya figo.

WHO imesema kwamba inatambua kwamba hospital ilioko Freeeport na Grand Bahama imefurika na maji yaliyochanganyika na maji taka na kwa hiyo inahitaji kuwepo mbadala kwenye uwanja

Timu za afya za kimataifa zinawasili  Bahamas kutoa huduma ya tiba na kusaidia manusura kupata chakula, maji salama na huduma za kujisafi.

Miongoni mwa vifaa vya msaada vinavyotolewa ni vyandarua kwa ajili ya kuweka paa kwa nyumba zilizoharibika.