Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nisipokuwa mhandisi au daktari basi nitakuwa mwalimu-Mtoto mkimbizi kambini Cox’s Bazar

Mtoto akisoma kitabu cha kiada kwenye kambi ya Cox's Bazar nchini Bangladesh (2 Julai 2019)
© UNICEF Patrick Brown
Mtoto akisoma kitabu cha kiada kwenye kambi ya Cox's Bazar nchini Bangladesh (2 Julai 2019)

Nisipokuwa mhandisi au daktari basi nitakuwa mwalimu-Mtoto mkimbizi kambini Cox’s Bazar

Wahamiaji na Wakimbizi

Mtoto mkimbizi kutoka Mynmar anayeishi Cox’s Bazar nchini Bangladesh amesema bila kujali mazingira anayoishi anataka kutimiza ndoto yake ya kusoma na kuwa mhandisi au daktari.

“Jina langu ni Shahed, nina umri wa miaka 12. Ninatoka Mynmar, tulikuja mwaka 2017”

Ni Shahed akijitambulisha na anasema ana umri wa miaka 12 na mara ya kwanza walipofika nchini Bangladesh mwaka 2017 kila kitu kilikuwa kipya kwake lakini sasa anajisikia vizuri.

Shahed anaishi katika kambi ya wakimbizi iliyo kubwa zaidi kuliko kambi zote za wakimbizi duniani, Cox's Bazar . Huku akitabasamu Shahed anasema,

(Sauti ya Shahed)

“Usipokuwa na elimu, basi unatakiwa kufanya kazi ngumu kama vile kuchimba mitaro. Bila elimu huwezi kupata kazi nzuri.”

Kwa wakimbizi, elimu ni moja ya mali pekee zinazohamishika. Shahed ameandikishwa katika mradi unaofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF akijifunza kuhusu nishati ya nguvu ya jua na na vifaa vya umeme. Bado anasisitiza umuhimu wa elimu,

(Sauti ya Shahed)

“Bila kuwa na elimu sahihi, kuna uwezekano mkubwa ukaanza kufanya uhalifu mdogomdogo. Kuna wizi na uporaji hapa. Ninaogopa.”

Wavulana barubaru wako katika hatari ya kutumia madawa ya kulevya na kujiunga na makundi. Shahed anasema anataka kuwa Mhandisi au daktari,

(Sauti ya Shahed)

“Lakini nikishindwa kufanya hivyo, basi nitaka kuwa mwalimu.”