Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafaniko yaliyopatikana ya karne ya maendeleo yanaweza kufutwa kwa usiku mmoja- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa 7 wa Tokyo kwa ajili ya maendeleo ya Afrika, TICAD VII, mjini Yokohama nchini Japan.
UN Japan/Ichiro Mae.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa 7 wa Tokyo kwa ajili ya maendeleo ya Afrika, TICAD VII, mjini Yokohama nchini Japan.

Mafaniko yaliyopatikana ya karne ya maendeleo yanaweza kufutwa kwa usiku mmoja- Guterres

Tabianchi na mazingira

“Hamna kitu kinaathiri maendeleo kama majanga”! Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres wakati akihutubia kikao cha Afrika kuhusu mabadiliko ya tabianchi kandoni mwa mkutano wa 7 wa Tokyo kwa ajili ya maendeleo ya Afrika, TICAD VII, mjini Yokohama nchini Japan.

Bwana Guterres amesema, “hatua za karne za maendeleo endelevu zinaweza kufutwa kwa usiku mmoja,” akitolea mfano vimbunga vilivyopiga Msumbiji mapema mwaka huu, mafuriko yaliyoikumba Japan siku chache zilizopita na moto zinazoshudiwa katika msitu wa Amazon.

Huku mwezi Julai ukitajwa kama mwezi wenye kiasi cha joto zaidi, Guterres amesema, “tuko njiani kwa miaka ya kati ya 2015 hadi 2019 kuwa miaka yenye joto zaidi duniani kuwa kurekodiwa wakati huo huo shirika la hali ya hewa duniani limeonyesha kwamba kuna viwango vya juu zaidi vya hewa ya ukaa kwenye mazingira katika historia.”

Katibu Mkuu huyo amesema waathirika wakubwa na wa kwanza ni watu maskini na walio hatarini akitaja kwamba Afrika ipo mstari wa mbele wa madhila kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi licha ya kwamba ni mchangiaji mdogo wa ongezeko la joto.

“Afrika ina mamlaka ya kimaadili kuhusu hilo,” Guterres amehimiza akiongeza kuwa Afrika ina haki ya kuwaomba nchi wenye uchangiaji mkuu wa gesi chafuzi kwenye mazingira ikiwemo China, Marekani na Idia kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira  kupunuguza viwango vya gesi chafuzi na kuendana na mapendekezo ya jamii ya wanasayansi kwa ajili ya kufikia dunia yenye vwango vya chini vya gesi chafuzi ifikapo mwaka 2050.

Kongamano la hatua dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi

Mnamo Septemba 23 mwaka huu, Katibu Mkuu ataandaa kongamano la hatua dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi mjini New York na mapendekezo ambayo tayari yamewasilishwa kulinda watu maskini na walio hatarini ikiwemo kuimarisha mbinu za kuibuka baada ya majanga na mbinu za kujiandaa kukabiliana na majanga.

Mmoja wa washriki wa kongamano hilo ni kijana Greta Thunberg, mchagizaji wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi na malengo ya maendeleo endelevu, SDGs mwenye umri wa miaka 16 kutoka Sweden ambaye amewasili New York, Marekani Jumatano Agosti 28 baada ya kusafiri kutoka Uingereza hadi Marekani kwa njia ya boti kama sehemu ya ujumbe wake kuhusu usafiri unaozingatia mazingira.

Greta Thunberg, mchagizaji wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi na malengo ya maendeleo endelevu, SDGs mwenye umri wa miaka 16 kutoka Sweden ambaye amewasili New York, Marekani Jumatano Agosti 28
UN Photo/Mark Garten)
Greta Thunberg, mchagizaji wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi na malengo ya maendeleo endelevu, SDGs mwenye umri wa miaka 16 kutoka Sweden ambaye amewasili New York, Marekani Jumatano Agosti 28

Bwana Guterres kupitia mtandao wa Twitter amemkaribisha Greta na kusema kwamba kujitolea kwake na kuvumilia safari hiyo kuanapaswa kuchagiza wale wote wanashirika katika kongamano la hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kufikia mahitaji ya wote kote ulimwenguni na kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi kote ulimwenguni.

Tweet URL

Moto wa Amazon

Kuhusu moto kwenye msitu wa mvua wa Amazon huko Amerika ya Kusini, Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa umechukua hatua kutoa kipaumbele kutatua akisema, “tumekuwa na mawasiliano na nchi kuona kama inawezekana wakati wa vikao vya ngazi ya juu kwenye Baraza la usalama kuwe na mkutano unaolenga kuchagiza msaada kwa ajili ya Amazon.