Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yasema si chembechembe zote za plastiki zina madhara kwa binadamu, lakini tafiti zaidi zahitajika

Chupa za plastiki pamoja na takataka katika kijiji kimoja kilichoko kando mwa mto na maji yake huishia katika bahari.
UN Photo/Martine Perret
Chupa za plastiki pamoja na takataka katika kijiji kimoja kilichoko kando mwa mto na maji yake huishia katika bahari.

WHO yasema si chembechembe zote za plastiki zina madhara kwa binadamu, lakini tafiti zaidi zahitajika

Afya

Chembechembe za plastiki ziko kila sehemu lakini havihatarishi afya ya binadamu limesema Shirika la afya ulimwenguni, WHO leo Alhamisi. Grace Kaneiya na maelezo zaidi.

WHO kupitia tafiti yake ya athari za uchafu wa chembechembe za  plastiki kwa binadamu limesema plastiki zimepatikana katika mazingira ya viumbe vya baharini, katika maji taka na maji safi, chakula na hewa na maji ya kunywa iwe ya chupa au bombani.

Kwa kawaida chembechembe hizo za plastiki ni zile ambazo ni chini ya milimita tano kwa urefu na idadi kubwa hupatikana katika maji ya kunywa vikitokana na vipande vidogo vya chupa za plastiki za maji.

WHO imesema kwa kuzingatia taarifa za sasa,  uwepo wa chembechembe hizo hauhatarishi afya kwa viwango vya sasa lakini utafiti zaidi unahitajil

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo Bruce Gordon kutoka kitengo cha afya ya umma, WHO amesema kwa sasa hatari kubwa kuliko chembechembe hizo za plastiki ni maji yasiyo safi na salama alama huku yakiathiri watu bilioni mbili duniani kote na kusababisha vifo vya watu milioni moja kila mwaka. 

Ameongeza kuwa muorobaini ni kuweka mifumo bora ya kuchuja maji na hivyo kupunguza uchafuzi wa plastiki ndogondogo kwa asilimia 90.

Bwana Gordon ameongeza kuwa watumiaji wa maji hawapaswi kuhofia sana lakini

SAUTI YA Gordon)

“Tunachagiza kufanyike mengi zaidi kupunguza uchafuzi utokanao na chembechembe hizo za plastiki na hiyo ni kutokana na wasiwasi kutokana na hali ya sasa tunayoshuhudia na inasikitisha na hiyo ni Zaidi ya utafiti wowote wa kiafya wa binadamu”.

Kwa upande wake Jenniffer de France kutoka kitengo cha afya ya umma cha WHO amesema kwa sasa utafiti umejikita katika maji ya kunywa huku akisema maji ya chupa yana chembechembe nyingi za plastiki ikilinganishwa na maji ya bomba lakini ametoa angalizo dhidi ya kufikia uamuzi kwani chembechembe zinazopatikana kwenye maji ya chupa za plastiki ni aina ya plastiki inayotumika kutengeneza chupa za plastiki na aina nyingine inatumika kutengeneza vikombe kwa hiyo utafiti Zaidi unahitajika kuelewa plastiki hizi zinatoka wapi.

Aidha ameongeza kuwa utafiti zaidi unahitajika

(Sauti ya Jenniffer)

“Ripoti hii imejikita na maji ya kunywa lakini ni muhimu kuzingatia maeneo mengine ya mazingira, kwa kutambua hilo, WHO tayari imeanzisha mchakato wa kufuatilia athari za kiafya kwa binadamu kwa kuwepo katika mazingira kunako plastiki.”