Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maji yaendelea kuchafuliwa, uhai wa jamii, uchumi wa nchi mashakani- Benki ya Dunia

Kisima kwenye kijiji cha  Dhokandpur nchini India ambako maji yanavunwa kwa matumizi ya nyumbani baada ya kupitishwa kwenye bomba.
UNDP India/Prashanth Vishwanatha
Kisima kwenye kijiji cha Dhokandpur nchini India ambako maji yanavunwa kwa matumizi ya nyumbani baada ya kupitishwa kwenye bomba.

Maji yaendelea kuchafuliwa, uhai wa jamii, uchumi wa nchi mashakani- Benki ya Dunia

Ukuaji wa Kiuchumi

Ubora wa maji unazidi kuwa duni kila uchao na kutishia uchumi wa nchi zinazoendelea ambako ndiko maji yamechafuliwa zaidi kwa chembechembe za plastiki, kemikali na vitu vinigne, imesema ripoti ya Benki ya Dunia iliyotolewa leo Jumanne. Ripoti hiyo imeonya pia kwamba janga lisiloonekana la viwango vya maji vinatishia uhai wa binadamu na mazingira

Moshi kwenye maji 

Katika baadhi ya maeneo, mito na maziwa yamechafuliwa na yanateketea mfano mzuri ni ziwa la Bellandur lililoko Bangalore, nchini India, ambalo limebeba majivu na kuyafikisha katika majengo yaliyoko umbali wa karibu maili sita.

Vyanzo vingine vya maji, hata hivyo vinachafuliwa kwa viwango vya chini lakini vinavyotishia huku ikiwa ni mchanganyiko wa bakteria, maji taka, kemikali na plastiki ambazo zinanyonya oksijeni kutoka kwa maji na kugeuza kuwa sumu.

Ripoti hiyo ya Benki ya Dunia ikipewa jina, Viwango visivyojulikana: Janga la maji lisiloonekana, linatoa mwanga kuhusu mchakato mpaka kufikia hapo kwa kutumia takwimu za viwango vya maji, vilivyokusanywa kutoka kwa vituo mbali mbali vya kufuatilia maji, na teknolojia za kutathmini kutoka mabli na mashine za mafunzo.

Ripoti imeonya kwamba bila hatua za haraka, viwango vya maji vitaendelea kuzorota na kuathiri afya ya binadamu, kupunguza uzalishaji wa chakula na hivyo kuathiri ukuaji wa uchumi.

Ukosefu wa Oksijeni

Maji apmoja na vitu vinavyochafua vikielekea kwenye mtaro, Maputo, Msumbiji.
Picha: John Hogg / World Bank
Maji apmoja na vitu vinavyochafua vikielekea kwenye mtaro, Maputo, Msumbiji.

Ripoti inakadiria kupungua kwa theluthi moja ya uwezo wa kiuchumi wa eneo kwa ajili ya viwango vya chini vya maji kutokana na vipimo vya oksijeni vinavyohitajika kibiolojia kwa ajili ya kutoa uchafu kwenye mazingira kutokana na uharibifu na bakteria wanaoishi katika vipimo maalum vya oksijeni kwenye mazingira.

Iwapo viwango vya oksijeni vinafikia viwango fulani, ukuaji wa uchumi katika maeneo ambako kuna maji yaliyoharibiwa vinapungua kwa theluthi moja kwa sababu ya athari mbaya dhidi ya afya, kilimo na mfumo wa ikolojia.

Naitrojeni ya kwenye mbolea nayo inadumaza ubongo wa watoto

Matumizi ya mbolea ya naitrojeni kwenye kilimo inatajwa kama moja ya changamoto kubwa katika kuhakikisha viwango vya juu vya maji kwani naitrojeni huingia katika mito, maziwa na bahari ambako inageuka kuwa naitreti.

"Naitreti ni sumu kwa watoto wachanga'" imeonya ripoti hiyo huku ikisema kuwa kemikali hiyo inaathiri ukuaji wao na ukuaji wa ubongo. Ripoti imesema kwa kila kilo moja ya nitrojeni kwa hekta moja inayoingia kwenye chanzo cha maji kama naitreti, idadi ya watoto wanaodumaa inaongezeka kwa hadi asilimia 19 ikilinganishwa na wale ambao hawakukutana na naitreti.

Hii pia ina athari kipato cha watoto hao katika siku za usoni huku ikipunguza mapato kwa asilimia hadi 12.

Chumvi nayo majini yapunguza rutuba kwenye udongo

Ripoti imesema pia ongezeko la viwango vya chumvi kwenye maji kutokana na hali ya ukame mkali, dhoruba na ongezeko la uchimbaji maji pia vimeangaziwa kama moja ya sababu inayofanya ardhi kupunguza uwezo wake wa kuzailisha mazao.

Ripoti inakadiria kwamba kila mwaka dunia inapoteza chakula kiwango ambacho kinaweza kulisha watu milioni 170 sawa na idadi ya watu nchini Bangladesh kutokana na ongezeko la chumvi kwenye maji.

Ili kukabiliana na changamoto hizo, Benki ya Dunia imetoa wito kuzingatiwe hatari hizo ambazo zinakumba mataifa yaliyoendelea na yale yanaendelea katika viwango vya kimatatifa, kitaifa na mashinani.

Ripoti inapendekeaza hatua ambazo nchi zinaweza kuchukua ili kuimarisha viwango vya maji ikiwemo sera za kimazingira na viwango: ufuatiliaji wa uhakika wa uchafuzi wa maji, mifumo thabiti ya utekelezaji, miundo mbinu ya kusafisha maji ikiungwa mkono na marupurupu ya kuchagiza uwekezaji binafsi na taarifa zilizo na uhakika, na zinazotegemewa kwa kaya ili kuvutia ushiriki wa raia.