Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Furaha yangu ni pale ninaposaidia kuokoa maisha ya wengine:Dkt.Mvumbi

Juni 20, mhudumu kutoka WHO anatoa chanjo kwa mwanaume nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC kijiji cha Bosolo
WHO/Lindsay Mackenzie
Juni 20, mhudumu kutoka WHO anatoa chanjo kwa mwanaume nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC kijiji cha Bosolo

Furaha yangu ni pale ninaposaidia kuokoa maisha ya wengine:Dkt.Mvumbi

Msaada wa Kibinadamu

Katika kuadhimisha siku hii ya kimataifa ya huduma za kibinadamu , moja ya nchi ambayo inahitaji kwa hali na mali huduma hizo ni Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, ambayo imeghubikwa na mjangamakubwa matano , kipindupindu, njaa, kutokuwa na uhakika wa chakula, vita nae bola.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa majanga hyo yamesababisha takribani watu milioni 12.8 kuhitaji msaada wa kibinadamu mwaka huu pekee wa 2019. Mashirika ya kibinadamu ya kitaifa na kimataifa na wahudumu wa kibinadamu wanahaha usiku na mchana kuhakikisha wananusuru maisha ya watu hao.

 Miongoni mwao ni Dkt.Gisele Mvumbi anayefanya kazi na shirika la afya ulimwenguni WHO nchini DRC kama kiongozi wa timu ya kudhibiti Ebola mjini Beni anaeleleza kinachompa furaha kama muhudumu wa kibinadamu, “Ahh! Ni pale tunapomuona mgonjwa amepona na kuondoka akiwa hai, ukweli tunapoweza kubaini maambukizi yao mapema na wanakuja katika kituo cha matibabu cha ebola ,na  kupata matibabu basi wanaondoka wakiwa wameponywa. Kwa sababu jamii inaamini kwamba tunapokuja ni dalili ya kifo. Ina changamoto, na endapo watakufa inakuwa kama juhudi zetu zote zimeenda bure. Lakini wakinusurika tunajivunia , tunawasindikiza wakati mwingine ma ngoma”

Ameongeza kuwa inapotokea hivyo tunafurahia sana na inawasaidia wagonjwa kuelewa kwamba watu wengine wanatoka wakiwa hai, na kuwaelewesha kwamba matibabu ya haraka yana matokeo tofauti kabisa ikilinganishwa na kuwasili kituoni kama wamechelewa. Giselle anasema na kinachomtoa huzuni,“ni pale ambapo hatueleweki , pale ambpo watu wanaturushia mawe tunapokuwa kazini, wakati panapokuwa na kifo, wakati ambapo tunatishwa na pia wakati tunapouawa, na hiyo sio sawa.Ni wajibu wetu kuleta mabadiliko, tunahitaji kuboresha vit una kufanya hali kuwa bora zaidi, mimi ni mtaalam katika kazi hii, hivyo ni wajibu wangu kufanya zaidi kuleta mabadiliko,kama tunafanya kwingine kwa nini isiwe hapa”?