Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya chanjo dhidi ya Ebola yaendelea nchini Burundi:WHO 

Uchunguzi wa virusi vya Ebola kwenye mpaka kati ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo , DRC na Uganda
WHO/Matt Taylor
Uchunguzi wa virusi vya Ebola kwenye mpaka kati ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo , DRC na Uganda

Kampeni ya chanjo dhidi ya Ebola yaendelea nchini Burundi:WHO 

Afya

Maandalizi na kampeni ya chanjo dhidi ya Ebola kwa mataifa jirani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambako ugonjwa huo bado unaendelea ni muhimu limesema shirika la afya duniani WHO. 

Nchi jirani ya Rwanda ilishachukua hatua madhubuti kwa kushirikiana na WHO na wadau wengine sasa juma hili Burundi imefuata nyayo ikianza na kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya wahudumu wa afya.

Mwakilishi wa WHO Burundi Dkt. Walter Kazadi anafafanua umuhimu wa kuendesha kampeni hiyo

(SAUTI YA DKT KAZADI CUT 1)

Ameongeza kuwa tangu Jumatano wiki hii ilipoanza rasmi kampeni hiyo  ambayo itaendelea hadi kila aliyekusudiwa apate chanjo ,wameshapiga hatua kubwa zikiwemo

(SAUTI YA DKT KAZADI)

Kampeni hii inatekelezwa chini ya usimamizi wa wizara ya afya ya umma na kudhibiti Ebola, ikishirikiana na shirika la afya duniani WHO. Na msaada wa kifedha wa kuendesha kampeni hiyo umetolewa na muungano wa chanjo duniani GAVI.

Burundi imepokea dozi za chanjo ya Ebola aina ya rVSV-ZEBOV kuwalinda wauguzi hao dhidi ya virusi vya Ebola aina ya Zaire ambavyo vimeiathiri DRC kwa hivi sasa.