Kuna sababu nyingi zinazochangia vijana kukosa elimu:UN

12 Agosti 2019

Umoja wa Mataifa umesema changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro ya mara kwa mara inayoshuhudiwa katika baadhi ya nchi ubora wa elimu, umasikini na hata mazingira vinakwamisha vijana wengi kupata elimu

Kando na changamoto hizo vijana ambao wanaishi na ulemavu wanakabiliwa na changamoto nyingine katika kufikia elimu kwa sababu ya ukosefu wa vifaa na hata teknolojia za kuwezesha kundi hilo kufikia jamii.

Kwa kutambua changamoto hiyo vijana nchini Tanzania katika shule ya Mvumi sekondari iliyopo mjini Dodoma wameanzisha klabu ya DCT inayowawezesha wanafunzi wanoishi na ulemavu kupata elimu Paul Mwame Sauli ni mwanzilishi wa klabu hiyo.

(Sauti ya Sauli)

Kwa upande wake Umoja wa Mataifa umeweka mkakati wa Vijana 2030 ili kuongeza ushiriki wake na vijana na kuwaunga mkono katika kufikia haki zao. Kwa kuzingatia hilo Umoja wa Mataifa ulimteua rais Uhuru Kenyatta kama kinara wa maswala ya vijana ambapo Walter Mong’are naibu mkurugenzi wa mawasiliano katika kitengo cha vijana kwenye ofisi ya rais katika mahojiano na Idhaa hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa amesema,

(Sauti ya Mongare)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud