Kila wiki mbili, lugha moja ya asili inapotea, wito wa kuzilinda watolewa

9 Agosti 2019

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya watu wa asili inayoazimishwa kila tarehe 9 Agosti ya kila mwaka, ambapo maadhimisho yanaenda sambamba na mwaka 2019 ambao ni mwaka wa kimataifa wa lugha za asili ikilenga kusaka hatua za haraka kulinda, kuchagiza na kuendeleza lugha za asili. 

Wito umetolewa duniani kote kuweka juhudi za kuzitunza lugha za asili.  Mathalani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema lugha ni jinsi ambavyo watu wanawasiliana na lugha ina uhusiano na tamaduni, historia na utambulisho.

Hata hivyo amesema licha ya umuhimu huo, nusu ya takribani lugha 6,700, idadi kubwa ikiwa ni zile za asili, ziko hatarini kutoweka. Guterresb ameesema, kwa kila lugha inayotoweka, dunia inapoteza utajiri wa tamaduni na ufahamu.

Pia wadau kupitia makala iliyoandaliwa na Grace Kaneiya, wametoa wito wa kuhakikisha uimarishaji wa lugha za kimataifa uendane sanjari na uhifadhi wa lugha za asili. 

\

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter