Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazao duni, ukosefu wa uhakika wa chakula unachochea uhamiaji Ukanda wa Amerika Kusini-WFP

Wakulima Guatema, Amerika ya kari wanakabiliana na athari za ukame.
WFP/Francisco Fion
Wakulima Guatema, Amerika ya kari wanakabiliana na athari za ukame.

Mazao duni, ukosefu wa uhakika wa chakula unachochea uhamiaji Ukanda wa Amerika Kusini-WFP

Tabianchi na mazingira

Kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo, hali ya hewa isiyotabirika, ukame wa muda mrefu na mvua kubwa zimeathiri mazao ya mahindi na maharagwe katika ukanda wa Amerika ya kati hali ambayo imeathiri pia uhakika wa chakula kwa wakulima wadogo huku wakikabiliwa na ugumu wa kulisha familia zao kila siku.

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema watu takriban milioni mbili nchini Guatemala, Honduras, El Salvador na Nicaragua wameathirika na milioni 1.4 kati yao wanahitaji msaada wa chakula haraka kwa muhibu wa utafiti wa shirika hilo mwishoni mwa mwaka jana 2018 na WFP na shirika la kilimo na chakula, FAO.

Jose Cirilo ni mkulima katika ukanda huo

(sauti ya Jose)

“Kwa sababu ya hali ilivyo hatukuweza kupanda chakula cha kutosha, ardhi haikuzalisha kama ilivyokuwa hapo awali na hiyo ilinilazimu kuhamia Marekani.”

Takriban asilimia 82 ya familia waliuza pembejeo zao na mifugo, na wakapunugza idadi ya mlo kwa siku na kula vyakula vyenye ubora mdogo wa lishe kama hatua ya kukabiliana na uhakika wa chakula huku vitendo kama hiyvo vikitajwa kama mbinu za kukabiliana na dharura.

WFP imesema wakulima wadogo wadogo katika ukanda huo wako hatarini na wakati wakipoteza mazao yao, wakulima hutafuta ajira katika mashamba ya karibu na mara nyingi hawana kipato kwa ajili ya kununua chakula.

Wakulima wengine wanahamia miji mingine , au nchi jirani au kwingineko. Miguel Baretto ni mkurugnezi wa WFP kanda ya Amerika Kusini.

(Sauti ya Miguel Baretto)

“Uhamiaji sio suluhu, wakati mtu anahama, wanaosalia nyuma wanakabiliwa na changamoto za uhamiaji. Inachukua muda wa miaka mitano kujikwamua kiuchumi wakati mtu mmoja anapohama, Kwa hiyo suluhu ni kufanya kazi pamoja kwa ajili ya mifumo ya muda mrefu ya chakula ambayo inaimarisha mnepo kwa wakulima na masoko bora”

Kwa mujibu wa WFP, takriban asilimia 25 ya kaya hazina kipato toshelezi kugharamia chakula cha msingi.

WFP inahitaji dola milioni 72 kupatia watu hao msaada wa chakula katika kipindi cha muda mfupi na kuwajengea uwezo wa kukabiliana na athari za muda mfupi na mrefu za mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha mifumo ya kitaifa ya kulinda jamii.