Nchi wanachama tumieni ushawishi wenu kupunguza machafuko Syria:ISSG

Familia ambazo zinakaa kambini karibu na mpaka na Uturukikufuatia uhasama unaoshuhusiwa jimbo la Idlib na Aleppo.(Juni 2019)
© UNICEF/UN0318979/Ashawi
Familia ambazo zinakaa kambini karibu na mpaka na Uturukikufuatia uhasama unaoshuhusiwa jimbo la Idlib na Aleppo.(Juni 2019)

Nchi wanachama tumieni ushawishi wenu kupunguza machafuko Syria:ISSG

Amani na Usalama

Jopo la kimataifa la msaada kwa ajili ya Syria (ISSG) leo limezitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kutumia ushawishi walio nao kusaidia kupunguza machafuko yanayoendelea Kaskazini Mashariki mwa Syria na kuongeza msaada muhimu wa kibinadamu unaohitajika nchini humo.

Wito huo umetolewa wakati wa mkutano wa kikosi kazi cha jopo hilo mjini Geneva Uswis na kuongeza kuwa“inasikitisha kwamba usitishaji wa uhasama uliotangazwa hapo awali ulisambaratika Jumatatu wiki hii na kwamba wimbi jipya la machafuko linatishia tena maisha ya mamilioni ya raia wanaoishi katika eneo la Idlib amba zaidi ya milioni moja ni watoto.”

Taarifa iliyotolewa na mshauri wa masuala ya kibinadamu wa mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifawa katika hali ya kibinadamu Syria imesema “wakati wa usitishaji mapigano raia wengi walirejea katika nyumba zao na sasa wako katika maeneo ambako mashambulizi makubwa yamerejea  na hivyo kuwaweka katika hatari kubwa.”

Familia zikiwa kwenye kambi ya muda, kilometa 50 kaskazini mwa Idlib nchini Syria. Tangu mwanzoni mwa Septemba 2018, maelfu ya watu wamefurushwa kutokana na kuongezeka kwa mapigano.
UNICEF/ Aaref Watad
Familia zikiwa kwenye kambi ya muda, kilometa 50 kaskazini mwa Idlib nchini Syria. Tangu mwanzoni mwa Septemba 2018, maelfu ya watu wamefurushwa kutokana na kuongezeka kwa mapigano.

Zaidi ya raia 500 wasio na hatia wameuawa na mamia wengine kujeruhiwa tangu kuanza kwa mapigano mwishoni mwa mwezi Aprili. 

Idadi ya watu waliotawanywa pia imeongezeka kwa kiwango cha kutisha ambapo wanaume, wanawake na Watoto 400,000 wamelazimika kukimbia kwa ajili ya usalama wao huku wengi ikiwa ni Zaidi ya mara moja wanafanya kivyo.

Idadi kubwa ya watu hawa wamekimbilia katika maeneo kuliko na watu wengi na wengine 30,000 zaidi wametawanywa katika maeneo ambayo yanadhibitiwa na serikali.

Taarifa hiyo imetaka urushaji wa makombora katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa serikali ya Syria ukome.

Mashambulizi ya anga na vifaru yamesababisha uharibifu mkubwa katika vituo vya afya, shule, masoko, vituo vya maji na miundombinu mingine ya raia. Na pande husika katika mfumo uliowekwa ili kuboresha usalama na ulinzi wa wahudumua wa misaada ya kibinadamu na operesheni za misaada , wametakiwa rasmi na Umoja wa Mataifa kutoa taarifa kuhusu matukio yaliyotokea Kaskazini Magharibi mwa Syria. Uturuki imejibu baadhi ya maombi , bado tunasubiri kusikia kutoka kwa shirikisho la Urusi” imesema taarifa hiyo.

Watoto wanaokimbia machafuko Idlib watafuta hifadhi kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani karibu na kijiji cha Atmeh.
UNICEF/Watad
Watoto wanaokimbia machafuko Idlib watafuta hifadhi kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani karibu na kijiji cha Atmeh.

 Wajibu wa kisheria kwa pande husika

Taarifa hiyo imesema pande husika katika mzozo zinabanwa kisheria kutekeleza wajibu wao chini ya sharia za kimataifa za kibinadamu na watekelezaji wa ukiukwaji wowote wa sharia za kimataifa za kibinadamu ni lazima wawajibishwe.

Kwa mujibu wa taarifa ya mshauri huoyo wahudumua wa masuala ya kibinadamu wanahofia taarifa inayoelezea uwezekano wa hatua za kijeshi kuingilia kati , jambo ambalo litakuwa na athari kubwa katika eneo hilo ambalo kwa miaka mingi tayari limeshashuhudia shughuli za kijeshi , watu kutawanywa, ukame na mafuriko. Na hivi karibuni eneo hilo liliathirika na moto ambao uliathiri mazao na uzalishaji wa kilimo.

Takribani watu 200,000 ni wakimbizi wa ndani huko Idlib nchini Syria kutokana na mapigano  yanayoendelea kwenye eneo hilo
@WFP Syria
Takribani watu 200,000 ni wakimbizi wa ndani huko Idlib nchini Syria kutokana na mapigano yanayoendelea kwenye eneo hilo

Usaidizi wa kibinadamu unaohitajika

Juhudi Zaidi zinahitajika imesema taarifa hiyo ili kuwasaidia watu milioni 1.6 wanaohitaji msaada wa haraka katika eneo hilo wakiwemo watu 604,000 ambao ni wakimbizi wa ndani na idadi yao inaendelea kuongezeka.

Msaada wa kibinadamu pia unapaswa kuendelea katika kambi ya Al Hol Kaskazini Magharibi ambako wanahifadhiwa watu 68,000 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto kutoka Syria na Iraq. 

Pia ripoti imesisitiza kwamba ulinzi bado ni suala linalotia wasiwasi na unahitaji kutolewa bila ubaguzi kwa kila anayeuhitaji na nchi wanachama zinapaswa kuchukua hatua kuhakikisha kwamba raia wao wanarejeshwa kwa kuzingatia viwango na sharia za kimataifa.

Taarifa za ndugu wasiojulikana waliko pia zinahitaji kutolewa kwa wapendwa wao wanaoishi kambini.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa hali bado ni tete na wote wenye ushawsihi katika mzozo wa Syria ni lazima wajitahidi kutatua mvutano huo.