Mexico inawajibika kwa tukio la mtu aliyepotea tangu mwaka 2010 - Wataalamu wa haki za binadamu

7 Agosti 2019

Mexico inatakiwa kufanya uchunguzi wa kina, huru na usioegemea upande kuhusu kutoweka kwa watu mnamo mwaka 2010, kamati ya haki za binadamu imeeleza katika maamuzi yaliyochapishwa leo mjini Geneva Uswisi.

Kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, kundi la wataalamu 18 wa kimataifa, imetangaza matokeo ya uchunguzi wao kwa kuzingatia sheria za kimtaifa za haki za binadamu baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa ndugu wa muathirika wa mtu aliyelazimishwa kutoweka. Kwa mujibu wa malalamiko, muathirika alikuwa akiendesha gari lake katika mji wa Poza Rica, Veracruz mnamo mwezi Oktoba mwaka 2010 wakati magari mawili ya polisi wa doria yalipomsimamisha na kumlazimisha chini yam tutu wa bunduki, kuingia katika moja ya magari yao. Baada ya mwenzake aliyeshuhudia tukio hilo, kumkosa katika vituo vyote vya polisi, yeye pamoja na ndugu wa aliyetoweka waliandikisha malalamiko yao. Msichana huyo aliwatambua maafisa watatu wa polisi kati ya wale waliohusika na tukio hilo lakini waliachiwa huru na kiongozi wao ambaye hata hivyo alikamatwa baadaye akihusishwa na kundi la uhalifu wa kupangwa la “Los Zetas.”

Kwa kuwa mamlaka za Mexico hawakufanya uchunguzi vya kutosha kuhusiana na kutoweka kwa mtu huyo, familia ya muathirika walileta malalamiko yao kwa kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ambayo ina mamlaka ya kuchunguza matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika nchi ambazo zimetia saini mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na kisiasa.

Ripoti ya kamati imeeleza kuwa ilibaini haki ya binadamu ya uhai, uhuru wa kutambulika mbele ya sheria na nyinginezo zimekiukwa na Mexico na kuwa hatua hazikuchukuliwa katika muda muafaka kiasi kilichosababisha kupotea kwa ushahidi muhimu na kuwa uchunguzi haukuwa huru, na uliegemea upande hivyo haukuweza kueleza kwa kina utowekaji wa mtu huyo na kuwatambua waliohusika.

“Ni muhimu kwa Mexico kuanza mchakato na kushinikiza wanaohusika na tukio hili ili kutokomeza muundo wa unaotekeleza matukio hayo nchini humo,” amesema  Hélène Tigroudja, mjumbe wa Kamati ya haki za binadamu.

Katika maamuzi yake, Kamati imeitaka Mexico kuripoti ndani ya siku 180, ikieleza hatua ambazo imezichukua ili kurekebisha hali.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud