Katibu Mkuu wa UN alaani mashambulizi na mauaji El Paso na Daytona nchini Marekani

5 Agosti 2019

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ametoa taarifa ya kulaani vikali mashambulio yaliyofanyika nchiin Marekani tarehe 3 mwezi huu wa Agosti na kusababisha vifo na majeruhi.

“Mashambulio hayo kwenye mji wa El Paso jimboni Texas na Dayton huko Ohio yamefanywa na watu wawili tofauti ndani ya saa chache” vimeripoti vyombo vya habari ambapo hadi sasa jumla ya watu 20 waliuawa kwenye shambulio la El Paso ilihali huko Daytona watu 9 akiwemo mshambuliaji mwenyewe na dada yake.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake jijini New York, Marekani, Bwana Gutereres ameeleza kushtushwa na kitendo hicho na kuelezea mshikamano wake na watu wa Marekani pamoja na serikali yao na serikali ya Mexico, ambayo idadi kubwa ya waliouawa na kujeruhiwa huko El Paso wanatoka taifa hilo la Amerika ya Kusini.

Katibu Mkuu amesisitiza umuhimu wa kila mtu kushirikiana na kudhibiti ghasia iliyoota mizizi kwenye chuki, ubaguzi wa rangi na aina zote zile za ubaguzi.

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud