Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waajiri wana wajibu wa kuweka mazingira bora kufanikisha unyonyeshaji wa mtoto-UNICEF Tanzania

Mama akinyonyesha mwanae nchini Tanzania
UN Photo/B Wolff
Mama akinyonyesha mwanae nchini Tanzania

Waajiri wana wajibu wa kuweka mazingira bora kufanikisha unyonyeshaji wa mtoto-UNICEF Tanzania

Afya

Umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto katika miezi sita ya kwanza ya maisha yake ni jambo ambalo linaendelea kusisitizwa kwa kutambua kwamba maziwa hayo sio tu ni lishe kamili kwa mtoto lakini yanasaidia kujenga afya ya mama na mtoto.

Licha ya jamii kuelewa umuhimu wa mama kumnyonyesha mtoto lakini bado kuna changamoto mbali mbali ambazo mara nyingi zinakwamisha utekelezaji wake kama anavyosema Tuzie Edwin, afisa wa lishe katika Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF Tanzania ambaye amesema moja ya changamoto ni suala la muda kwa akina mama ambao wanafanya kazi na hivyo ni muhimu kwa muajiri kuweka mazingira ambamo mfanyakazi ataweza kumnyonyesha mtoto au kukamua maziwa akitolea mfano wa shirika lake

(Sauti ya Tuzie)

“UNICEF tuna chumba maalum kwa ajili ya akina mama kunyonysha watoto wao lakini pia kukamua maziwa. Tumezingatia mazingira ambayo ni rafiki kwa mama na mtoto pia.

UNICEF sio tu inaongoza kwa vitendo lakini imetoa ujumbe mahsusi kwa wadau husika

“Tunaasa jamii, familia na serikali kuhamasiha mazingira rafiki kwenye sehemu za kazi ili kufanikisha unyonyeshaji wa watoto.”

Wiki ya unyonyeshaji watoto huadhimishwa kila mwaka kuanzia Agosti 1 hadi na kufikia kilele tarehe 7.