Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP Tanzania yaonesha njia, yazindua mfumo wa nishati jua kwenye jengo lake Dar es Salaam

Paneli za sola ambazo zimetegwa tayari kukusanya nishati hiyo endelevu.
Shutterstock
Paneli za sola ambazo zimetegwa tayari kukusanya nishati hiyo endelevu.

UNDP Tanzania yaonesha njia, yazindua mfumo wa nishati jua kwenye jengo lake Dar es Salaam

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP nchini Tanzania leo limezindua mfumo wa umeme jua uliofungwa katika ofisi zake, maeneo ya Oyster bay, jijini Dar es Salaam, ukizalisha megawati 187 kwa mwaka.

UNDP  inasema kuwa kiwango hicho cha umeme kitokanacho na paneli 696 zenye uwezo wa kuzalisha kilowati 227, kinakuwa ni kikubwa zaidi kufungwa katika sehemu moja nchini Tanzania ambapo utasaidia kupunguza gharama za matumizi ya umeme na kuchangia katika kutunza na kuhifadhi mazingira.

Akizungumza baada ya uzinduzi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Tanzania Dkt. Hamisi Mwinyimvua amesema ubia wa UNDP na serikali unafanikisha malengo ya kufikisha nishati kwa wote na kwamba,

(Sauti ya Dkt. Hamisi Mwinyimvua)

 Naye mtaalamu wa teknolojia wa UNDP Tanzania Leyla N’Doman, akifafanua amesema kwenye hilo jengo lao, matumizi ya umeme wa TANESCO yatakuwa ni asilimia 30 ilhali asilimia 70 itakuwa ni nishati  ya jua na kwamba..

 (Sauti ya Leyla)