Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taasisi ya Benjamin Mkapa yasaidia kuimarisha huduma za afya vijijini- Dkt. Ellen

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi  ya Mkapa, Hellen Mkondya Senkoro akihojiwa na Arnold Kayanda wa UN News kando mwa mkutano wa CSW63.
UN News/Patrick Newman
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa, Hellen Mkondya Senkoro akihojiwa na Arnold Kayanda wa UN News kando mwa mkutano wa CSW63.

Taasisi ya Benjamin Mkapa yasaidia kuimarisha huduma za afya vijijini- Dkt. Ellen

Afya

Taasisi za kiraia zimeendelea kushirikiana na serikali hususan katika nchi zinazoendelea ili kuweka mazingira bora ya kazi maeneo ya vijijini kwa wahudumu wa afya na hivyo kufanikisha lengo namba 3 la malengo ya maendeleo endelevu kuhusu afya bora na ustawi kwa wote.

Miongoni mwa taasisi hizo ni ile ya Benjamin Mkapa nchini Tanzania ambayo kwa kushirikiana na serikali ina miradi mbali mbali ya kuhakikisha wakazi wa vijini wanapata huduma ya afya na watoa huduma nao wanavutiwa kufanya kazi maeneo hayo kama anavyofafanua Dkt Ellen Mkondya Senkoro, Afisa Mtendaji Mkuu kwenye taasisi hiyo alipohojiwa mapema mwaka huu na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

(Sauti ya Dkt. Ellen)

"Wahudumu wa afya wanapokea maandalizi ili kuwaanda kufanya kazi katika mazingira ya viijijini kwani mazingira ni tofauti. Wanapokea fursa ya kufahamu waendako na nini cha kutarajia."

Kando na kuwaandaa watoa huduma lakini pia taasisi hiyo inahakikisha kwamba wasimamizi wa watoa huduma nao wamepokea mafunzo na maandalizi wanayohitaji kama anavyoeleza Dkt. Ellen

(Sauti ya Dkt. Ellen)

"Kando na mafunzo wa wahudumu wa  afya, wasimamizi nao wanapokea mafunzo ili kuwawezesha kufanikisha kazi lakini pia kuwasaidia wahudumu wa afya kuimarisha stadi zao ni kukua katika kazi zao."