Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres atuma salam za rambirambi kwa familia za waathirika wa tetemeko huko China

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
TASS/ UN DPI
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Guterres atuma salam za rambirambi kwa familia za waathirika wa tetemeko huko China

Tabianchi na mazingira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametuma salam zake za rambiramibi kwa familia ya waliopoteza maisha kufuatia tetemeko la ardhi kusini mwa jimbo la China la Guizhou kufuatia mvua kubwa.

Bwana Antonio Guterres kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Jumapili ameelezea kusikitishwa kwake na vifo, uharibifu wa mali kufuatia tetemeko la ardhi.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, takriban watu 36 wanashukiwa kupoteza maisha kufuatia tetemeko hilo lililotokea Jumanne katika kijiji cha Pingdi kaunti ya Shuicheng.

Tangu wakati huo timu za kuokoa watu zinajaribu kutafuta manusura kwa kuchimba idongo kw akutumia mashine.

Kwa mujibu wa ripoti watu arobaini wamekwisha okolewa lakini wengine 15 hawajulikani waliko kwnai nyumba 20 zilifunikwa na udongo.

Bwana Guterres amewapongeza timu ya uokozi na operesheni zinazofanywa na serikali ya China, wakati mvua zikiendelea kushuhudiwa huku akielezea utayari wa Umoja wa Mataifa kutoa msaada wake katika juhudi hizo.

Matetemeko ya ardhi sio nadrwa kwa maeneo ya vijijini na milima katika sehemu za China, hususan baada ya mvua kubwa; nchi hiyo imekabiliwa na mafuriko makubwa mwaka huu.