Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA kutoa muongozo wa matumizi ya mionzi kutibu saratani ya wanyama

Muuguzi akipima kiwango cha mionzi
UN
Muuguzi akipima kiwango cha mionzi

IAEA kutoa muongozo wa matumizi ya mionzi kutibu saratani ya wanyama

Afya

Matumizi ya mionzi katika tiba ya wanyama yanaongezeka kila siku duniani kote huku Shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA likitoa utaratibu kwa madaktari wa mifugo kuhusu namna ya kutumia nguvu za nyuklia kwa usalama.

 

Kwa mujibu wa IAEA kupitia video yake iliyochapishwa kwenye wavuti wake, wanayama pia huumwa saratani na hivyo kuna haja ya kuwachunguza na kuwatibu kwa kutumia mionzi. Eberhard Lubewig ni kutoka chuo kikuu cha tiba ya mifugo, Vienna nchini Austria na anasema

(SAUTI YA LUBEWIG)

“Tunatibu mifugo wengi, kuanzia wanyama wadogo kama ndege na jamii ya mijusi hadi wanayama wakubwa na wazito kwa mfano farasi na ng’ombe na wanyama wengine wanaopatikana kwenye mbuga za wanyama.”

IAEA inasema utaratibu wa kutibu wanyama na binadamu ni tofauti kwa mfano katika matumizi ya mionzi ya jua, wanyama wanahitaji dawa ya kuwalaza ili kuwawezesha madaktari wa mifugo kuweza kuwahudumia huku uchunguzi na upigaji picha za x-ray ukifanyika nje ya hospitali, huku wamiliki wa mifugo na wahudumu wa afya ya mifugo wakihitajika kushika wanyama watulie na kupata matibabu. Bwana Lubewig ameongeza

(SAUTI YA LUBEWIG)

“Iwapo ni muhimu watu wawe chumbani wakati wa uchunguzi, basi ni muhimu kupunguza dozi ya matibabu.”

Aidha vifaa vya usalama ni muhimu katika kuhakikisha kuwalinda wahudumu wa afya kutokana na mionzi

IAEA kwa sasa inaandaa ripoti yake ya kwanza kuhusu usalama na kujikinga dhidi ya mionzi kwa wahudumu wa afya ya wanyama Debbie Gilley ni mtaalam wa ulinzi dhidi ya mionzi

(SAUTI YA DEBBIE)

“Kwa kawaida wanyama hawafuati maagizo vizuri, kwa hiyo tuna changamoto ya kuhakikisha wanafuata maagizo kwa ajili ya uchunguzi hata mdogo kwa hivyo hii ilikuwa ni jibu kwa kutoa utaratibu kwa halmashauri ya usimamizi na wahudumu wa afya ya wanyama kuhusu mbinu za kutumia mionzi kwa njia salama.”