Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaendelea kupambana na njaa na utapiamlo

Mtoto huyu pichani mwenye umri wa miezi miwili ni mkazi wa Hajjah, nchini Yemen na ana unyafuzi. Mzozo unaoendelea nchini Yemen unasababisha mamilioni ya watu wawe hatarini kukumbwa na baa la njaa.
WFP/Marco Frattini
Mtoto huyu pichani mwenye umri wa miezi miwili ni mkazi wa Hajjah, nchini Yemen na ana unyafuzi. Mzozo unaoendelea nchini Yemen unasababisha mamilioni ya watu wawe hatarini kukumbwa na baa la njaa.

FAO yaendelea kupambana na njaa na utapiamlo

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Ukaguzi wa kina kuhusu wajibu ya FAO katika kupaambana na njaa na utapiamlo tangu mwaka 2012 na  utafiti kuhusu changamoto kwa ajenda hii ya mwongo mmoja uanaokuja utafanyika katika kituo cha FAO cha Sheikh Zayed tarehe Ijumaa yatehe 26 mwezi huu wa Julai.  Jason Nyakundi anayo taarifa kamili

Warsha hiyo ambayo itaongozwa na washidi wa tuzo la Kimataifa ya chakula ya mwaka 2018, Lawrence Haddad na David Nabarro, itatambua kazi na kujitolea kwa mkurugenzi mkuu wa FAO José Graziano da Silva dhidi ya kutokomeza njaa.

Itazungumzia njia bora za kukabiliana na njaa na utapiamlo kwa njia zote huku changamoto zinazotokana na utipwatipwa zikipewa kipaumbele.

Wazungumzaji ni pamoja na wawakilishi wakuu kutoka shitrila la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), shirika la Afya Duniani (WHO), Jopo linalohusika na kilimo, mifumo ya chakula na lishe (GLOPAN), Vuguvugu linaloboresha lishe (SUN), Muunano unaohusika na magonjwa yasiyoambukiza (NCD) na muungano wa kimataifa kuhusu lishe iliyoboreshwa (GAIN).

Kufanikisha lengo la usalama wa chakula kwa wote ifikapo mwaka 2030 ndicho kuingo muhimu katika lengo namba 2 ya maendeleo endelevu.

Hii ni pamoja na kutokomeza aina zote za uhaba wa lishe ambazo kwa wakati huu zinawaathiri zaidi ya watu bilioni 2 huku zaidi ya watoto milioni 14 wakikubwa na tatizo la kukua. Hii inamaanisha pia kukabiliana na utipwatipwa unaowaadhiri takriban mtu mmoja kati ya watu 8 duniani.