Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana Tanzania wakumbatia mifuko mbadala wa plastiki kulinda mazingira na kujipatia kipato

Mfuko wa plastiki.
UNnewskiswahili/Patrick Newman
Mfuko wa plastiki.

Vijana Tanzania wakumbatia mifuko mbadala wa plastiki kulinda mazingira na kujipatia kipato

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Wakati serikali ya Tanzania inaendelea na utekelezaji wa hatua ya kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki kwa ajili ya kulinda mazingira , hatua hiyo inaleta neema kwa vijana walioamua kujifunza utengenezaji wa mifuko mbadala.

Mafunzo ya utengenezaji wa mifuko ya karatasi yanatolewa na vyuo mbalimbali na kwa vijana wanajitokeza kwa wingi kwani mbali ya kuhifadhi mazingira kwao ni ajira na inawapa kipato. Miongoni mwa vijana hao ni mwanafunzi wa sekondari kidato cha tano Charles Michael Samweli ambaye yeyé na wanafunzi wenzie wamejikusanya na sasa wanaendesha biashara ya kutengeneza na kuuza mifuko hiyo kwa hiyo gharama nafuu jijini Dar es Salaam. Akizungumza na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa  Dar es Salaam Tanzania Charles anamesema

(SAUTI YA CHARLES MICHAEL SAMWELI)

Kazi yao bado ni changa changamoto zake ni zipi?

(SAUTI YA CHARLES MICHAEL SAMWELI)

Je wanafaidikaje?

(SAUTI CHERLES MICHAEL SAMWELI)