Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauzo ya hewa ya ukaa ni ushindi kwa uhifadhi wa mazingira na kipato  Kenya-UN Environment

Mikoko baharini
Maktaba
Mikoko baharini

Mauzo ya hewa ya ukaa ni ushindi kwa uhifadhi wa mazingira na kipato  Kenya-UN Environment

Ukuaji wa Kiuchumi

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UN Environment, halmashauri ya misitu Kenya na taasisi ya utafiti ya viumbe baharí na samaki Kenya na wadau hivi karibuni wamezindua mradi katika pwani ya Kenya kwa ajili ya kukuza biashara ya hewa ya mkaa kufuatia uhifadhi na upanzi wa mikoko. Flora Nducha na taarifa zaidi

Taarifa ya UN Environment iliyotolewa Nairobi, Kenya, inasema kuwa wakati kunapatikana mfumo wa kuhifadhi mazingira na unaopunguza umasikini na kujengea jamii mnepo kiuchumi, kwa kawaida serikali hupiga jeki hatua kama hizo na kwa hiyo ni suluhu ya ushindi kwa pande zote.

Ripoti zinasema kuwa kwa  sasa kuna upungufu wa mikoko kwa sababu ilikuwa inavunwa kupita kiasi kwa ajili ya kuni na mbao za ujenzi, hali ambayo inazua hatari kwani jamii nyingi zinazotegemea uvuvi, huku maeneo ya mikoko yakiwa ni maeneo ya mazalia ya samaki. 

Mwasiti Salim ni mkazi wa kijiji cha Vanga kunakoendeshwa mradi huu.

(Sauti ya Mwasiti Salim)

Kando na kuhakikisha uhakika wa chakula na njia za kujipatia kipato lakini mikoko ina muhimu katika kuzuia mawimbi makali na pia ni ngao kwa maeneo ya vijiji vinavyopakana na misitu mingine. 

Faida zaidi ni kama anavyoelezea  James Kairo kutoka taasisi ya viumbe maji na samaki Kenya.

(Sauti ya James Kairo)

"Unapoathiri mikoko, unaathiri nyasi majini, miamba ya matumbwe na samaki na unaathiri viumbe vya majini kwa ujumla. Mikoko ni muhimu sana katika kunasa na kuhifadhi hewa ya ukaa. Kwa hiyo wakati msitu wa mikoko unaharibiwa, hewa ya ukaa inaingia kwenye anga na tunashuhudia mabadiliko ya tabianchi. Kazi yetu sasa ni kunasa hewa chafuzi ya ukaa na kuiuza katika soko la hewa ya ukaa. Tuko hapa kujaribu mifumo ya kuimarisha hewa ya ukaa kwa ajili ya kukuza na kuimarisha msitu.”

Mauzo ya hewa ya ukaa yatasaidia wakazi vijijini kuimarisha kipato na pia kukidhi mahitaji ya familia zao. 

Haridh Mohammed naye pia ni mkazi wa kijiji cha Vanga kunakotarajiwa kuanzishwa mradi huu.

(Sauti ya Haridh)

Wakazi wanasubiri kwa hamu ujio wa mradi na kwa lao ni dua tu, Mwasiti tena

(Sauti ya Mwasiti)