Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN na Liberia watia saini makubaliano ya uchangiaji wa vikosi vya ulinzi wa amani.

Eneo katika kambi ya kijeshi ya MINUSMA baada ya kushambuliwa kwa mnano Mei 3 2017, tukio ambalo lilisababisha kifo cha mlinda amani mmoja kutoka Liberia na kuwajerhi wengine kadhaa.
UN Photo/Sylvain Liechti
Eneo katika kambi ya kijeshi ya MINUSMA baada ya kushambuliwa kwa mnano Mei 3 2017, tukio ambalo lilisababisha kifo cha mlinda amani mmoja kutoka Liberia na kuwajerhi wengine kadhaa.

UN na Liberia watia saini makubaliano ya uchangiaji wa vikosi vya ulinzi wa amani.

Amani na Usalama

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya operesheni za amani mashinani Atul Khare na mwakilishi wa kudumu wa Liberia katika Umoja wa Mataifa Balozi Dee-Maxwell Saah Kemayah, mjini New York  Marekani  wametia saini makubaliano ya kutambua mchango wa vikosi vya ulinzi wa amani kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu Mali, MINUSMA. Ujumbe huo wenye walinda amani 105 umekuwa ukihudumu huko Timbuktu tangu Oktoba mwaka 2016.

Liberia tangu mwaka 1993 imekuwa mwenyeji wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa ukiwemo mpango wa ulinzi wa amani wa kuanzia mwezi Septemba mwaka 2003 hadi Machi 2018. Kwa kutia saini makubaliano haya, Liberia sasa rasmi imehama kutoka kuchangiwa vikosi na sasa kuwa mchangiaji wa walinzi wa amani katika operesheni za Umoja wa Mataifa tofauti na hapo awali ambapo yenyewe ndiyo ilikuwa ikisaidiwa kurejeshewa amani.

Wakati wa hafla ya utiaji saini, Bwana Khare amesema kuwa, “Mapito ya Liberia kuelekea kwenye amani yanaonesha mchango chanya wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa kama nchi ambayo imehama kutoka katika mgogoro kwenda katika utulivu na leo ni mdau muhimu katika kusaidia nchi nyingine zenye uhitaji.”

Naye Balozi Dee-Maxwell Saah Kemayah Sr amesema, “utiwaji saini wa makubaliano haya kati ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Liberia ni wa muhimu sana kwani unasisitiza ahadi kati ya serikali ya Liberia kupitia vikosi vya kijeshi vya Liberia na Umoja wa Mataifa katika mipango ya kulinda amani kwenye MINUSMA.”

On this important occasion, the UN pays tribute to the service and sacrifice of Liberian peacekeeper Ousmane Ansu Sherif, who lost his life in an attack on a MINUSMA camp in Timbuktu on May 2017.

Aidha Umoja wa Mataifa umelitumia tukio hili muhimu kuonesha kutambua na kuheshimu huduma na kujitolea kwa mlinda amani Ousmane Ansu Sherif ambaye alipoteza maisha  katika shambulizi lilifanyika mnamo mwezi Mei mwaka 2017 katika kambi ya MINUSMA huko Timbuktu nchini Mali. 

Liberia inachangia wanajeshi 118, kati yao asilimia 10.6 wakiwa ni wanawake ambao wanahudumu katika mpango wa MINUSMA Mali na UNMISS huko Sudan Kusini. Liberia iko katika nafasi ya 68 kati ya nchi wanachama 122 wa Umoja wa Mataifa  ambao wanachangia wanajeshi katika vikosi vya ulinzi wa amani.

Kwa sasa Umoja wa Mataifa una makubaliano 321 kati yake na nchi 80.