Watunga sera chukueni hatua kunusuru vijana wa vijijini- IFAD

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ujumbe wa Umoja wa Mataifa MINUSCA unatekeleza mradi wa matokeo ya haraka ya kuwezesha jamii kupata kipato na kujinusuru na umaskini.
UN/MINUSCA - Hervé Serefio
Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ujumbe wa Umoja wa Mataifa MINUSCA unatekeleza mradi wa matokeo ya haraka ya kuwezesha jamii kupata kipato na kujinusuru na umaskini.

Watunga sera chukueni hatua kunusuru vijana wa vijijini- IFAD

Ukuaji wa Kiuchumi

Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD umesema sera bora na uwekevaji vinahitajika haraka ili nchi maskini ziweze kupatia mustakabali bora mamilioni ya vijana wao maskini wanaoishi vijijini.

Sauti na taswira za vijana kutoka maeneo mbalimbali ya dunia.. ni kwenye video mahsusi ya mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD, iliyochapishwa kuangazia ni kwa vipi kundi hili la vijana hususan waishio vijijini linapaswa kuangaziwa ili lijikwamue kiuchumi.

IFADI kupitia ripoti yake ya maendeleo vijijini yam waka 2019 inasema kuwa takribani vijana milioni 500, karibu nusu ya vijana katika nchi zinazoendelea, wanaishi vijiini.

Vijana hawa kwa mujibu wa IFAD wako hatarini kutumbukia kwenye lindi la umaskini na ukosefu wa usawa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa stadi za kazi, ukosefu wa ardhi, mitaji na kutokuunganishwa na mitandao ya kijamii.

Ripoti inasema kuwa kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, idadi ya vijana wa vijijini inatarajiwa kuongezeka kutoka milioni 105 mwaka 2015 hadi milioni 174 mwaka 2050 huku nchi hizo zikiwa hazina mbinu za kukabiliana na changamoto za usoni zitokanazo na ongezeko la idadi hiyo.

Gilbert Houngbo ni Rais wa IFAD na anasema. "iwapo hatutachakua hatua mahsusi, tutalazimika kuendelea kukabiliana uhamiaji wa lazima wa kusaka fursa za kiuchumi na hatari ya ongezeko la ukosefu wa usawa na hali tete itokanayo na hamahama hiyo.”

Ripoti imeonesha kuwa vijana waishio vijijini, na maeneo ya viunga vya mijini asilimia 67 kati yao wanaishi kwenye maeneo bora ya kilimo lakini wengi wao hawana fursa za masoko.

IFAD imeonya kuwa watunga sera lazima wachukue hatua kuepusha janga kubwa zaidi ikitaja athari za kilimo kwa mabadiliko ya tabianchi na kutumia fursa itokanayo na maendeleo ya teknolojia.