Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amano alijitahidi kuhakikisha nyuklia inatumika kwa usalama:Guterres

Aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa IAEA Yukiya Amano akikutana na mgonjwa wa saratani katika taasisi ya uchunguzi na tiba ya  saratani ya Ocean Road (ORCI)Tanzania
IAEA/Conleth Brady
Aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa IAEA Yukiya Amano akikutana na mgonjwa wa saratani katika taasisi ya uchunguzi na tiba ya saratani ya Ocean Road (ORCI)Tanzania

Amano alijitahidi kuhakikisha nyuklia inatumika kwa usalama:Guterres

Masuala ya UM

Yukiya Amano alifanyakazi bila kuchoka kuhakikisha nishati ya nyuklia inatumika tu kwa sababu salama. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika tarifa yake kufuatia kifo cha mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomiki IAEA.

Guterres katika tarifa hiyo iliyotolewa na msemaji wake amesema “Nilishtushwa sana mapema leo asubuhi kupokea tarifa za kifo cha Bwana Yukiya Amano.”

Guterres amesema kwa takriban muongo mmoja Amano ameliongoza shirika la IAEA kwa mfano wa kuigwa , kwani ameboresha afya za watu kupitia juhudi za matumizi ya nyuklia kutengeneza dawa n atiba, kwa binadamu, katika kilimo na maeneo mengine muhimu.

Mbali ya uongozi bora Katibu Mkuu amesema Amano alikabiliana na changamoto kubwa duniani zikiwemo zile zinazohusiana na uzalishaji wa silaha za nyuklia na akazihimili kwa ubora wa hali ya ju una ari kubwa, na kwa ajili hiyo “dunia yetu sasa bi bora zaidi”

Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Bwana Amano na wafanyakazi wote wa IAEA na kusema “tukiomboleza pigo kubwa la kumpoteza , pia tunamshukuru Bwana Amano kwa huduma yake kwa taifa lake na binadamu wote.”