Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uharibifu wa makazi ya wapalestina unakiuka mapendekezo ya ICJ- Taarifa ya pamoja

Msichana mwenye umri wa miaka mitatu anayeonekana pichani, yeye na familia yake wamelazimika kuyahama makazi yao mara tatu katika mwaka mmoja tu wa 2018
UNRWA/Lara Jonasdottir
Msichana mwenye umri wa miaka mitatu anayeonekana pichani, yeye na familia yake wamelazimika kuyahama makazi yao mara tatu katika mwaka mmoja tu wa 2018

Uharibifu wa makazi ya wapalestina unakiuka mapendekezo ya ICJ- Taarifa ya pamoja

Haki za binadamu

Taarifa ya pamoja ya Jamie McGoldrick, mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo linalokaliwa la wapalestina, Bi. Gwyn Lewis mkurugenzi wa operesheni za shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA na bwana James Heenan mkuu wa ofisi ya haki za bindamu katika ofisi ya maeneo yaliyokaliwa ya Palestina imesema wanafuatilia kwa karibu kwa huzuni kubwa na uharibifu wa makazi ya wapalestina katika eneo la Sur Bahir.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa leo, maelezo ya  awali kutoka kwa jamii yanaonyesha kwamba mamia ya vikosi vya Israeli waliingia katika makazi ya jamii na kuharibu nyumba ikiwemo ambazo zilikuwa ni makazi ya watu zilizoko maeneo ya A, B na C ya ghuba ya magharibi mpakani nwa  Mashariki mwa Yerusalem.

Taarifa hiyo imesema operesheni hizo zimeanza alfajiri wakati bado kukiwa na giza ambapo familia zililazimika kukumbia na kusababisha wasi wasi mkubwa kwa wakazi. Miongoni mwa waliolazimika kukimbia au waathirika ni wakimbizi wa kipalestina ambao wengi wanafurushwa kwa mara ya pili.

Watoa huduma wa misaada ya kibinadamu wanatarajiwa kuwasilisha misaada kwa waathirika wa uharibifu huo wa mali binafsi. Hata hivyo taarifa ya wakuu hao imesema hakina msaada wa kiasi chochote ambao unaweza kurudisha makazi au kugharamia uharibifu mkubwa wa kifedha ambao umewakumba watu hao.

Kwa mujibu wa taarifa yao wengi wa watu walioathirika wamesema walikuwa wamewekeza akiba yao ya maisha katika kujenga kufuatia kupata idhini kutoka kwa mamlaka ya Palestina.

Taarifa hiyo ya pamoja imekumbusha kwamba uharibifu wa mali za wa Palestina unakiuka sheria za kimataifa ambapo uharibifu wa mali katika maeneo yaliyokaliwa unaruhusiwa tu pale ikiwa ni lazima kwa ajili ya operesheni za kijeshi ambapo kwa wakati huu hailkubaliki. Isitoshe inasababisha kufurushwa kwa lazima kwa wapalestina walio ghuba ya magharibi ikiwemo mashariki mwa Yerusalem.

Mwaka 2014 mahakama ya kimataifa ya haki ICJ ilitoa uamuzi dhidi ya ujenzi wa kizuizi na kusema kwamba sehemu ya vizuizi katika ukingo wa Magharibi ikiwemo mashariki mwa Yerusalem kwa mfano katika maeneo ya Sur Bahir hauwezi kuhalalishwa na unakiuka wajibu wa Israeli chini ya sheria za kimataifa.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Julai 20, mwaka 2004 ilitaka Israel kuzingatia wajibu wake na kufuata mapendekezo ya ICJ kupitia azimio namba ES-10/15, la 20 Julai 2004.