Tunashikamana na watu wa Japan kufuatia shambulio la Kyoto:UN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema leo kwamba maeshitushwa sana na vifo vya watu takriban 33 ndani ya studio maarufu ya vikaragosi mjini Tokyo vilivyosababishwa na shambulio la maksudi la moto ambalo limeelezwa kuwa moja ya mashambulio mabaya zaidi lililoua watu wengi katika historia ya Japan.
Polisi nchini Japan sasa wamembaini mtu anayeshukiwa kufanya shambulio hilo Alhamisi asubuhi ambaye ameroipotiwa kuingia katika jenngo la studio hiyo ya vikaragosi la Kyoto, KyoAni akiwa amebeba makopo ya bidhaa za majimaji za mlipuko ambayo aliyamwaga katika sehemu tofauti za studio hiyo kabla ya kuliwasha moto.
Kwa mujibu wa duru za Habari , walioshuhudia mtu huyo akikamatwa wamesema alisikika akidai kwamba kampuni hiyo ya vikaragosi iliiba baadhi ya fikra au mawazo yake ya ubunifu. Takriban watu 70 walikuwa ndani ya jingo hilo wakati moto uliolipuka kwa kasi ulipoanza na watu zaidi ya 30 walikimbizwa hospitali na wengi wa waliokufa wanadaiwa kukutwa kwenye ngazi wakijaribu kukimbia moto huo mkubwa.
“Katibu Mkuu ameshitushwa sana na kupotea kwa maisha ya watu kutokana na shambulio la moto mjini Kyoto” imesema taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya msemaji wake na “ametuma salamu za rambirambi kwa waathirika, watu na serikali ya Japani pia amewatakia ahuweni ya haraka majeruhi wote”.
Bwana Guterres ameongeza kwamba “Katika kipindi hiki cha janga kubwa, Umoja wa Mataifa unashikamana na serikali na watu wa Japan.”
Duru za Habari zinasema watu wengi wamejitokeza leo ijumaa nje Kyoto nje ya jingo hilo na kuonyesha heshima zao kwa kuweka maua na kusali.
Kampuni hiyo ya vikaragosi imeshatengeneza picha nyingi za video ambapo hivi karimuni simema yake ya vikaragosi mfululizo ijulikanayo kama Violet Evergarden imechukuliwa na warusha vipindi wengi duniani kwenye mtandao lakini pia kuonyeshwa na kampuni ya Netflix.