Watu milioni 2 wahitaji msaada wa chakula kufuatia ukame Zimbabwe:WFP

19 Julai 2019

Asilimia 38 ya watu wote wanaoishi vijijini nchini Zimbabwe sawa na takribani watu milioni 3.5 kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu wa mavuno Septemba 2019 hawana uhakika wa chakula kutokana na ukame wa mara kwa mara.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP idadi hiyo imetokana na tathimini ya hali ya chakula iliyofanywa nchini humo na kamati ya serikali na wadau wengine  kubaini hali ya chakula ZimVAC, hasa maeneo ya vijijini.

WFP imeongeza kuwa taifa hilo lenye jumla ya watu milioni 14.5, tathimini imekadiria kwamba hali ya kutokuwa na uhakika wa chakula itakuwa mbaya zaidi na kuathiri asilimia 50 ya kaya zote vijijini ambapo watu zaidi ya milioni 5.5hawatakuwa na uhakika wa chakula wakati wa kipindi cha njaa kali cha msimu wa muambo kuanzia Januari hadi Machi 2020.

Kamati ya ZimVAC inajumuisha serikali, Mmashirika ya Umoja wa Mataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali, NGOs na mashirika mengine ya kimataifa  na tathimini hiyo ya Maisha vijijini huijulisha serikali na wadau wengine wa maendeleo kuhusu mipango ya maendeleo vijijini nchini Zimbabwe na WFP ina jukumu kubvwa katika mradi huo ikichangia fedha na tathimini ya kiufundi .Msemaji wa WFP Geneva ni Hervey Verhoosel anasema

Mwanamke akitembea katika moja ya nyumba 2000 zilizoharibiwa na kimbunga idai kilichopiga kambi ya  Tongogara kusini mashariki mwa Zimbabwe.
UNHCR/Zinyange Auntony
Mwanamke akitembea katika moja ya nyumba 2000 zilizoharibiwa na kimbunga idai kilichopiga kambi ya Tongogara kusini mashariki mwa Zimbabwe.

"Matarajio haya ya kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na uhakika wa chakula kwa watu zaidi ya milioni 5.5 katika kaya za vijijini ni sawa na ongezeko la asilimi 138 ya kutokuwa na uhakika wa chakula ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka jana, n ani ongezeko la asilimia 73.9 kutoka kiwango cha wastani kwa kipindi cha miaka mitano.”

Kwa mantiki hiyo amesema WFP imechukua hatua“Kwa kuzingatia kiwango na ukubwa wa hali ya kutokuwepo na uhakika wa chakula nchini Zimbabwe , WFP imepanga kuongeza msaada wake kwa watu zaidi ya milioni 2 hadi kufikia kilele cha msimu wa muambo 2019-2020 ambao ni kati ya Januari mpaka Aprili 2010.”

Amesema hadi wakati huo timu za WFP zitaendelea kufanya kazi ili kusambaza mgao wa dahrira wa chakula kwa makundi ya watu wasiojiweza huku pia wakishirikiana kwa karibu na jamii kujenga mnepo dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi na zahma zingine siku za usoni.

Jumla ya fedha za ufadhili ambazo WFP inazihitaji ili kukidhi mahitaji haya katika mfumo wa utekelezaji wa miezi 9 ni dola milioni 173. Katika muongo mmoja uliopita Zimbabwe imekuwa ikishuhudia changamoto kubwa za kiuchumi na kimazingira ambazo zimechangia nchi hiyo kuingizwa katika orodha ya kimataifa ya njaa kwa mwaka 2015 ikisema kwamba taifa hilo liko katika kiwango cha hatari kubwa kuwa kwenye hatari kubwa na asilimia 62.6 ya watu wake wanaishi katika kiwango cha chini ya umasikini uliokithiri.

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter