Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana Sudan Kusini pambaneni michezoni lakini sio vitani:UNMISS

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umekamilisha ujenzi wa uwanja wa kandanda nje kidogo ya mji wa Juba lengo kuu likiwa kuwaunganisha wanajamii kupitia michezo.
UNMISS

Amani na Usalama

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umekamilisha ujenzi wa uwanja wa kandanda nje kidogo ya mji wa Juba lengo kuu likiwa kuwaunganisha wanajamii kupitia michezo.

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umekamilisha ujenzi wa uwanja wa ndanda nje kidoyo ya mji wa Juba lengi kuu likiwa kuwaunganisha wanajamii kupitia michezo. 

Katika uwanja wa mpira wa miguu nje yam ji mkuu wa sudan Juba, mechi iliyokuwa ukisubiriwa kwa
hamu sasa imeanza, timu mbili kutoka klabu ya Kor Romla zinachuana katika uwanja huu mpya uliojengwa kwa msaada wa walinda amani wa UNMIS kutoka Thailand na Nepal.

Wasakata gozi waliokumbana na visiki na makorongo uwanjani n ahata kushindwa kufurahia mchezo
waupendao inaponyesha mvua sasa wanafuraha na matumaini makubwa akiwemo Uhuru Peter Okimo

(SAUTI YA UHURU PETER OKIMO-KAMAU)
“Uwanja huu utachagiza amani katika jamii yangu katika njia ambayo sisi kama jamii tutatuma barua na tutakuwa na mashindano mbalimbali na jamii totautitofauti.”

 Wakiangalia mechi hii ya kwanza kabisa katika uwanja huu wanajumuiya wanamatumaini kwamba kandanda itwasasaidia
kuweka kando tofauti zao. Christopher Ladu ni mwenyekiti wa timu ya Kor Romla

(SAUTI YA CHRISTOPHER-JASON)

“Michezo ni hatua chanya katika shughuli za jamii, kutokana na hali ya nchi yetu ya Sudan kusini, watu wametawanyika
na kuwakusanya ili waishi pamoja itawezekana kupitia michezo.”

 Mbali ya uwanja wa soka Kamanda wa UNMISS Juba Brigedia Jenerali Eugene Nkubito anasema walinda amani pia wamewatengenezea
uwanja wa voleboli  na kuwagawia vifaa mbalimbali ya micezo na UNMISS inaamini kwamba michezo mbali ya kuwaburudisha itawapunguzia vijana fikra za kushiriki vita na kuwaunganisha.

(SAUTI YA JENERALI EUGENE NKUBITO-KIBEGO)

Miradi kama hii itakuwa ni msingi wa amani Jamhuri ya Sudan Kusini. Msaada kwa klabu hizi hautokuwa na faida ya kimwili tu ya kucheza , bali pia faida ya afya ya akili kwa watu.”