Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wanahitaji tiba mahsusi kukabiliana na ebola-UNICEF

Mtoa huduma katika kituo cha matibabu Butembo akiwa na mtoto ambaye mama yake alifariki kutokana na ugonjwa wa ebola siku chache zilizopita, Kivu Kaskazini mwa Jamhuri ya Kidmokrasia ya Kongo.
UNICEF/Vincent Tremeau
Mtoa huduma katika kituo cha matibabu Butembo akiwa na mtoto ambaye mama yake alifariki kutokana na ugonjwa wa ebola siku chache zilizopita, Kivu Kaskazini mwa Jamhuri ya Kidmokrasia ya Kongo.

Watoto wanahitaji tiba mahsusi kukabiliana na ebola-UNICEF

Afya

Watoto ni miongoni mwa waathirika wakubwa wa mlipuko wa ugonjwa wa ebola ambapo kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, kufikia Julai 7 kulikuwa na maambukizi ya visa 750 miongoni mwa watoto.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi, msemaji wa UNICEF  Marixie Mercado amesema katika ziara yake hivi karibuni nchini Jamhuri ya Kidmeokrasia ya Kongo ametembelea majimbo mawili ya Kivu Kaskazini na Ituri ambako kunashuhudiwa mlipuko wa ebola.

 Bi Mercado amesema watoto hususan wa chini ya umri wa miaka mitano wameathirika vibaya huku asilimia 40 ya visa 750 ni kutoka kundi hilo.

 UNICEF imesema hali hiyo inaweka hatarini wanawake ambao wameambukizwa na watoto idadi ikiwa ni asilimia 57 ya visa vyote.

 Ili kuzuia maambukizi ya ebola miongoni mwa Watoto UNICEF imesema ni lazima iwe ni kiini cha juhudi zote za kukbailiana na gonjwa hilo na kwamna watoto wanahitaji tiba mahsusi kwa sababu unaathiri watoto kwa njia tofauti na hivyo juhudi za kukabiliana nao zinahitaji kuzingatia mahitaji ya kisaikolojia na kijamii.

 Aidha Bi Mercado amesema kuwa watoto wanaotenganishwa na wazazi wao kwa sababu ya Ebola wanahitaji kutunzwa wakati wazazi wao wakipokea matibabu.

UNICEF kwa sasa wana wauguzi wa watoto katika vituo vya ebola wanaotota tiba kwa watooto na kila mtoto anapata mlezi ambaye ni manusura wa ugonjwa wa ebola.

Aidha UNICEF imewekeza katika vifaa tiba na masuala ya lishe kwa ajili ya watoot waathirika wa ebola.