Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika Kusini ‘kidedea’ katika kupunguza maambukizi mapya ya VVU- Ripoti

Gloria ambaye anaishi na virusi vya ukimwi katika vitongoji vya Khayelitsha mji wa Cape Town, Afrika Kusini ambako kampeni ya kuchagiza uelewa wa ukimwi ilifanyika mnamo Agosti 2007.
World Bank/Trevor Samson
Gloria ambaye anaishi na virusi vya ukimwi katika vitongoji vya Khayelitsha mji wa Cape Town, Afrika Kusini ambako kampeni ya kuchagiza uelewa wa ukimwi ilifanyika mnamo Agosti 2007.

Afrika Kusini ‘kidedea’ katika kupunguza maambukizi mapya ya VVU- Ripoti

Afya

Kasi ya maendeleo ya kupunguza maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi, VVU, kasi ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa dawa na kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi inapungua, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ukimwi, UNAIDS. 

Tunahitaji kuchukua dharura ya usimamizi wa kisiasa ili kumaliza ugonjwa wa Ukimwi, alisema Gunilla Carlsson Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS.

Bi. Carlson amesema  kuwa hii inaanza na uwekezaji mzuri na kile kinachangia nchi zingine kufanikiwa.

 Amesema "kumaliza Ukimwi ni suala lilonawezekana ikiwa tutaangazia watu kuliko ugonjwa, kujenga barabara kwa watu na meeneo yaliyoachwa nyuma na kutumia mbinu chini  ya misingi ya haki za binadamu kuwafikia watu walioathiriwa zaidi na virusi vya Ukimwi."

Ripoti hiyo inaonesha kuwa watu wazima na wapenzi wao huchukua nusu ya asilimia 54 na maambukizi mapya ya HIV kote duniani.

Mwaka 2018 watu wakiwemo wanaojidunga madawa, mashoga na wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wengine, watu waliobadili jinsia, makahaba na wafungwa, walichukua asilimia 95 ya maambuzia mapya ya VVU mashariki mwa Ulaya na kati kati mwa Asia na pia mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika.

Hata hivyo ripoti hiyo pia inaonesha kuwa ni chini ya  asilimia 50 ya watu hao ndio walifikiwa na huduma za kuzuia VVU katika zaidi ya nusu ya nchi zilizoripoti. Hii inaonyesha kuwa watu hawa bado wanatengwa na kuachwa nyumba katika vita dhidi ya VVU.

Kote duniani watu milioni 1.7 waliambukizwa upya virusi vya ukimwi mwaka 2018, kupungua kwa asilimia 16 tangu mwaka 2010 ikiwa ni kutokana na hatua zilizopigwa eneo la mashariki na kusini mwa Afrika.

Muelimishaji rika Arafah akizungumza na kundi la wanafunzi wa shule huku akisambaza vifaa vya kuelimisha kuhusu VVU na Ukimwi huko Khartoum, Sudan
UNICEF/SUDA2014-XX166/Noorani
Muelimishaji rika Arafah akizungumza na kundi la wanafunzi wa shule huku akisambaza vifaa vya kuelimisha kuhusu VVU na Ukimwi huko Khartoum, Sudan

Afrika Kusini kwa mfano imepiga hatua kubwa na imefanikiwa kupunguza maambukizi mapya ya VVU  kwa zaidi ya asilimia 40 na vifo vinavyotokana na ugonjwa wa ukimwi kwa karibu asilimia 40 tangu mwaka 2010.

Hata hivyo kuna safari ndefu kwa maeneo ya mashariki na kusini mwa Afrika, eneo lilioathirika zaidi na HIV, na pia kuna ongezeko la kutia wasi wasi katika maambukizi mapya ya VVU mashariki mwa Ulaya na kati kati mwa Asia, katika asilimia 29, mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika asilimia 10 na Amerika ya Kusini asilimia 7.

Ripoti hiyo ilizinduliwa katika warsha moja ya kijamii huko Eshowe, Afrika Kusini na Bi .Carlsson na David Mabuza, makamu wa Rais wa Afrika Kusini.

Ufadhili

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa mwanya katika mahitaji ya ufadhili na upatikanaji wake unazidi kuwa mkubwa. Kwa mara ya kwanza ufadhili unaopatikana kupamba na Ukimwi ulipungua sana kwa karibu dola bilioni moja.

Mwaka 2018 dola za kimarekani bilioni 19 zilipatikana kwa vita dhidi ya Ukimwi, upungufu wa dola bilioni 7.2 katika makadirio ya dola bilioni 26.2 zilizohitajika ifikapo mwaka 2020.

Katika kuendela na jitihada za kumaliza ugonjwa wa ukimwi, UNAIDS inawashauri washirika wote kuchukua hatua na kuwekeza, ikiwemo ufadhili  kamili kwa Mfuko wa Kimataifa kupambana na Ukimwi, kifuo kikuu na Malaria kwa takriban dola bilioni 14.

Vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi

Vifo vinavyotokana na ugonjw wa Ukimwi vinazidi kupungua huku huduma za matibabu zikiendelea kuongezeka na hatua zaidi zinapigwa katika kutoa huduma dhidi ya VVU na kifua kikuu. Tangu mwaka 2010 vifo vinavyotokana na Ukimwi vimepungua kwa asilimia 33 hadi 770 000 mwaka 2018.

Mafanikio huwa ni tofauti kimaeneo. Kipungua kimataifa kwenye vifo vinavyohusiana na ukimwi imetokana kwa kiwango kikubwa na hatua zilizopigwa mashariki na kusini mwa Afrika

Mashariki mwa Ulaya na kati kati mwa Asia hata hivyo, vivyo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi vimeongezeka kwa asilimia 5 mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika kwa asiliamia 9 tangu mwaka 2010.

Mtoto mchanga akitolewa sampuli za damu ili apimwe VVU katika moja ya vitu vya kuchunguza Virusi Vya Ukimwi, VVU huko Kyrgyzstan
UNICEF/Aleksei Osipov
Mtoto mchanga akitolewa sampuli za damu ili apimwe VVU katika moja ya vitu vya kuchunguza Virusi Vya Ukimwi, VVU huko Kyrgyzstan

Watoto

Karibu asilimia 82 ya wanawake wajawazito wanaoishi na VVU wanapata madawa ya kupunguza makali ya Ukimwi, ongezka la zaidi ya asilimia 90 tangu mwaka 2010.

Hii imechangia kupungua kwa asilimia 41 katika maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa watoto huku kupungua zaidi kukishuhudiwa nchini Botswana kwa asilimia 85, Rwanda (83%), Malawi (76%), Namibia (71%), Zimbabwe (69%) na Uganda (65%) tangu 2010.

Lakini kulikuwa na maambukizi mapya 160,000 ya VVU miongoni mwa watoto kote duniani mbali sana na lengo la kupunguza maambukizi mapya miongoni mwa watoto hadi chini ya 40,000 ifikapo 2018.

Mengi yanahitajika kufanywa kuongeza matibabu kwa watoto. Idadi ya takriban watoto 940,000 walio na umri kati ya miaka 0 na 14 wanaoishi na VVU kote duniani mwaka 2018 ni karibu mara dufu idadi ya mwaka 2010.

Wanawake na wasichana waliobalehe

Licha ya bado kuwepo pengo kubwa kati ya wanawake na wanaume wachanga, huku wanawake wachanga wakiwa wameambukizwa kwa asilimia 60 kuliko wanaume wachanga wa umri sawa, kumekuwa na mafanikio katika kupunguza maambukizi miongoni kwa wanawake wachanga.

Kote duniani maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa wanawake wachanga walio na umri wa miaka kati ya 15 na 24 yalipungua kwa asiliamia 25 kati ya mwaka 2010 na 2018, ikilinganishwa na kupungua kwa asilimi 10 miongoni mwa wanawake wa umri mkubwa walio na umri wa miaka 25 na zaidi.

Kuzuia VVU

Jamii husika zinaonyesha kuwa mbinu kadhaa zilizopo kwa kuzuia maambukizi ya VVU hazitumiki ipasavyo.

Kwa mfano matumizi ya dawa ya pre-exposure prophylaxis (PrEP), ya kuzuia VVU ilikuwa inatumiwa na takriban watu 300,000 mwaka 2018, 130,000 kati yao wakiwa nchini Marekani.

Nchini Kenya, moja ya nchi za kwanza za Kusini mwa Jangwa la Sahara kuanza matumizi ya dawa ya PrEP kama program ya kitaifa, karibu watu 30,000 waliipaga dawa hiyo ya kujikinga mwaka 2018.

Unyanyapaa na ubaguzi

Mafanikio yamepatikana dhidi ya unyanyapaa unaohusu VVU na ubaguzi katika nchi nyingi lakini tabia za kibaguzi dhidi ya watu wanaoishi na VVU bado ziko juu.

Ripoti pia inasema kuwa kuna hitaji la dharura kupata suluhu la ubaguzi na vuzuizi katika kuzuia na kwa matibaua ya VVU. Kama hiyo haitoshi ripoti imesema kuwa tabia za kibaguzi dhidi ya watu wanaoishi na VVU ni za juu katika nchi nyingi. Kwenye nchi 26 zaidi ya nusu ya watu waliohojiwa walikiri kuwa na hisia za kibaguzi dhidi ya watu wanaoishi na VVU.