Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kudaka mpira katika uwanja wa kriketi ni rahisi, kudaka mnyama ni mtihani:Mkimbizi Hashimi 

Kondoo.
Photo: FAO/Marco Longari
Kondoo.

Kudaka mpira katika uwanja wa kriketi ni rahisi, kudaka mnyama ni mtihani:Mkimbizi Hashimi 

Wahamiaji na Wakimbizi

Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza walinena wahenga , japo wakati mwingine inaweza kuwa nuru ya kuangaza mambo mapya. Kutana na muomba hifadhi Saad Hashmi kutoka Pakistan aliyepata fursa ya kutembelea shamba la ufugaji kondoo huko Yorkshire nchini Uingereza, kipi kilijiri ungana na Flora Nducha

Hapa katika shamba la ufugaji kondoo mjini Yorkshire mfugaji Rodney Beresford amekaribisha wageni shambani kwake ambao ni wakimbizi na waomba hifadhi.  Kwa wakimbizi nchini Uingereaza kupata fursa kama hii ya kutembelea shambani inaweza kuwa chachu ya mabadiliko ya maisha yao na kujifunza kitu kipya.

Mfuko wa hisani wa Yorkshire Dales Millennium Trust kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR,  kila mwaka huandaa ziara za wakimbizi na waoomba hifadhi kutembelea sehemu mbalimbali mashinani ambako wanaweza kujitolea na kujifunza ikiwemo katika shamba hili la kufuga kondoo ambalo leo kazi kubwa ni kuweka chapa kwa kondoo ambayo si kazi rahisi.

Miongoni mwa washiriki zoezi hili ni Saad Hashmi muomba hifadhi kutoka Pakistan anayehusudu mchezo wa kriketi

(SAUTI YA SAAD HASHMI-KAMAU)

“Ni kazi ngumu mi nacheza sana kriketi na naweza kudaka mpira , lakini kudaka mnyama ni kazi ngungu”

Rodney aliyefungua mlango wa zizi lake kwa wakimbizi na waomba hifadhi hawa anasema

“Baadhi yao wanakuja na hawajawahi kubeba kondoo kabisa au lolote lilanofanana na hilo , na wanajishangaa kwa kile wanachoweza kufanya.”

Safari hizi huwasaidia sana waomba hifadhi kama Hashmi kuchangia na pia kushirikiana na jamii wakati wakisubiri maombi yao ya hifadhi kushughulikiwa

(SAUTI YA  SAAD HASHMI-KAMAU)

“Kwa minajili ya afya ya akili ya waomba hifadhi na wakimbizi, matukio kama haya yanasaidia.”

Na afisa wa Yorkshire Dales Millenium Trust Judy Rogers anasema watu hawa

(SAUTI YA JUDY ROGERS-AMINA)

“Hawawezi kufanya kazi hivyo waomba hifadhi wengi wamechoka kukaa bure, wanapenda kujitolea kufanya vitu, lakini pia kutoka nje kwani hawapati fursa hiyo.”

Kwa wakimbizi na waomba hifadhi hii pia ni ni fursa ya kutoka nje ya mji, kujifunza ufugaji wa kondoo na kuyafahamu maeneo ya mashambani ya Yorkshire.