Skip to main content

Programu ya mamilioni ya dola kuwapatia elimu zaidi ya watoto 54,000 walioathirika na mgogoro nchini Somaliland yazinduliwa.

Ukosefu mkubwa wa ajira na elimu nchini Somaliland umewafanya maelfu ya vijana wadogo kuhama eneo hilo kila mwezi.
IRIN/Mohamed Amin Jibril
Ukosefu mkubwa wa ajira na elimu nchini Somaliland umewafanya maelfu ya vijana wadogo kuhama eneo hilo kila mwezi.

Programu ya mamilioni ya dola kuwapatia elimu zaidi ya watoto 54,000 walioathirika na mgogoro nchini Somaliland yazinduliwa.

Utamaduni na Elimu

Shirika la Umoja wa Mataifa, kwa kushirikiana na serikali ya Somaliland na mradi wa Elimu haiwezi kusubiri, hii leo mjini Hargeisa wamezindua programu ya miaka mitatu ya kuongeza upatikanaji wa elimu bora kwa watoto na vijana walioathiriwa na mgogoro unaoendelea nchini Somaliland.

Mradi wa ‘Elimu haiwezi kusubiri’ unachangia dola milioni 6.7 kuanzisha shughuli zilizopangwa na pia kuongeza chachu katika michango kutoka kwa wachangiaji wengine kukamilisha dola milioni 57.3 zilizosalia na zinazohitajika kutekeleza programu nzima ya miaka mitatu.

Makamu wa rais wa Somaliland, Abdirahman Abdillahi Ismail amesema“serikali ya Somaliland inajivulia kushirikiana na mradi wa ‘Elimu haiwezi kusubiri’ ECW. Kwa uwepo wa zaidi ya asilimia hamsini ya watoto nje ya shule, uwekezaji wa ECW utasaidia wasichana na wavulana 18,000 kwa mwaka kuweza kupata huduma ya elimu bora itakayowapatia maarifa na ujuzi kwa ajili ya mchango chanya katika maendeleo ya jamii, siasa na uchumi.”

Upatikanaji wa elimu nchini Somaliland ni unafikiwa na watu wachache ambapo wastani wa mahudhuro kitaifa unaonesha kwa ngazi ya msingi ni asilimia 49 kwa wavulana na asilimia 40 kwa wasichana. Watoto wa Somaliland ndiyo wameathirika zaidi kwani inaonekana asilimia 51 ya watoto wako nje ya mfumo wa shule.

“Tumejizatiti kutimiza haki ya lengo la SDG namba nne au elimu bora kwa watoto na vijana wote wa Somaliland. Ni wakati wao, kujifunza, kukua, kuendelea na kufanikiwa.” Amesema Yasmine Sherif, Mkurugezi wa mradi wa Elimu hauwezi kusubiri.