Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinazoendelea hazipaswi kuwajibika na uzalishaji wa uzalishaji wa hewa chafuzi uliotokea tangu zamani

Ndege iliyopewa jina United Dream ikiwa na mapambo yanayohamasisha SDGs
Xiamen Airlines
Ndege iliyopewa jina United Dream ikiwa na mapambo yanayohamasisha SDGs

Nchi zinazoendelea hazipaswi kuwajibika na uzalishaji wa uzalishaji wa hewa chafuzi uliotokea tangu zamani

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Ijumaa ya leo mjini New York Marekani, akiangazia mabadiliko ya tabianchi kwa kuzingatia yanasababishwa na “uzalishaji wa hewa chafuzi kwa kipindi cha tangu zamani”, mkuu wa shirika la anga la Xiamen la China, Bwana Zhao Dong amelieleza baraza la juu la kila mwaka la Umoja wa Mataifa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (HLPF) kuwa wazalishaji wakubwa wa hewa ukaa wanatakiwa kuchukua wajibu mkubwa zaidi kurekebisha tatizo.

“Kama mwakilishi wa tasnia ya usafiri wa anga, tunaamini kwamba ni muhimu kusongeshga mbele hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutekeleza mkataba wa Paris.” Bwana Zhao ameeleza katika mjadala kuhusu lengo namba 13 la SDG linalohusu mabadiliko ya tabianchi akieleza kama sababu kwa nini miaka miwili iyopita alitia saini makubaliano na Umoja wa Mataifa kuifanya Xiamen kuwa “shirika la anga la kwanza duniani kuunga mkono malengo ya maendeleo endevu, SDGs”.

Kwa hali ilivyo na mabadiliko ya tabianchi yanavyoonesha kote duniani, mabadiliko ya joto, mabadiliko ya misimu na kuongezeka kwa mabadiliko makubwa ya hali ya hewa, vinatishia maono yay a viongozi wa dunia waliyoayafikia mjini Paris kuhusu kudhibiti mabadiliko ya tabianchi ikiwa lengo ni kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030.

Matokeo ya mabadiliko ya tabianchi ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa, yanaweka changamoto kwa usafiri na tasnia ya usafiri wa anga.

Tweet URL

 

Kwa mujibu wa ripoti ya mazingira ya shirika la kimataifa la anga la Umoja wa Mataifa ICIAO, kuongezeka kwa joto la Dunia kulikosababishwa na uzalishaji wa hewa  chafuzi utaathiri uwezo wa ndege kupaa na pia kuongezeka kwa kina cha bahari kutaathiri viwanja vya ndege.

Baada ya Xiamen kusaini makubaliano na Umoja wa Mataifa chini ya muongozi wa malengo 17 ya maendeleo endelevu, shirika hilo la ndege lilianzisha miradi 12 katika vipengele vine vya “usalama endelevu, uzalishaji mdogo wa hewa ya ukaa, ‘huduma ya kijani’ na mgawanyo wa faida”.

Bwana Zhao amewaambia washiriki kuwa kwa sasa shirika lao linaangalia uwezekano wa kuachana na vitu vya plastiki katika ndege zao na wanafikiria pengine kuanza kutumia vikombe vinavyotokana na miti ya mianzi.